ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 18, 2014

MGOMBEA URAIS WA DMV NDG. LIBERATUS MWANG’OMBE "LIBE" ATEMBELEA HOSPITALI TANZANIA 2011 na 2013

Na Liberatus Mwang'ombe

Liberatus believes "CHARITY STARTS AT HOME"


 Katika muendelezo wa kusaidia nyumbani kama imani yangu ya kimsingi; ninaamini kuwa, “binadamu tulizaliwa tushirikiane na tusaidiane kutatua matatizo na sio kutengana wala kushindana.” Kwenye safari yangu ya Tanzania 2011 na 2013 nilipata fursa ya kutembelea hospital za Muhimbili na Aga Khani zilizopo Dar Es Salaam, na hospital ya Muhimbira iliyopo kijijini kwetu Chimala, Mbeya.   Kwenye hospital ya Muhimbili na Aga Khan niliongozana na Dr. Leslie Kingslaw (A Pulmonologist from Wshington Hospital and Providence Hospital) na Ms. Kingslow (Nurse practitioner). 
 
Dr. Kingslow akiendelea kutoa somo la ugonjwa wa COPD
Aga Khan
                                 Muhimbili na Aga Khan, year 2011

Katika safari hii Dr. Kingslaw alitoa somo juu ya ugonjwa wa Chronic Obstractive Pulmonary Disease (COPD) unao sababishwa na uvutaji wa sigara kwa asilimia kati ya 80-90%.  Ugonjwa huu husababishwa pia na mambo mengine, kama vile, genes, historia ya familia, kazi unayofanya na mazingira; lakini husababishwa na utumiaji tumbaku (sigara) kwa asilimia kati ya 80-90%.

Libe akiwa hospital ya muhimbili  katikati ni Dr. Kingslow na Nurse kabla ya lecture
Libe akiwa na Mr. & Ms. Kingslow na daktari wa Aga Khan baada ya lecture
Baada ya kutoa somo juu ya gonjwa hili, COPD, tuliweza kutoa vipimo vya oxygen kama msaada.  Vipimo hivyo vinaitwa “pulse oximetry”.  Vile vile nilipata kubadirishana mawazo na madaktari wa Muhimbili na Aga Khan.  Katika mabadirishano ya mawazo; nilishtushwa na ukweli kuwa kuna watu hupoteza maisha kwa sababu tu, hawawezi kulipia mtungi wa oxygen! Baada ya mazungumzo hayo; nilirudi USA na kuendelea kupiga “box” huku nikitafakari jinsi ya kutatua matatizo haya.  Bado tafakuri hili linaendelea na naomba ushirikiano wa waTanzania wote waliopo USA kufanya jambo lolote kwaajili ya nyumbani.

Safari ya hospital ya Muhimbira Chimala Mbeya, year 2013

Juu na chini Liberatus anarudisha kidogo alicho nacho kwenye hospital ya kijijini kwao

Hii ni kati ya hospital masikini nilizo tembelea.  Niliona mengi ambayo yanatakiwa kuwezeshwa.  Hospital ya Muhimbila hutoa huduma kwa watu zaidi ya 20,000 kwa mwaka! Hospitali hii inaupungufu wa vifaa mbalimbali vya kutendea kazi; kama vile, vitanda, sindano, dawa za maleria, vipimo vya X-ray, oxygen tanks n. k.  Hii ni hospital niliyo kuwa natibiwa maleria kipindi nikiwa mdogo.  Sikusita kupita na kutoa kidogo nilicho jaliwa.  Nilipo enda nyumbani mwaka 2011 waliniambia kuwa wanaupungufu wa vifa vya kutendea kazi, kama vile  kipimo cha “Blood Presssure”.  Mwaka 2013 nilipo kwenda niliwapelekea kipimo hicho cha mapigo ya damu na chenye uwezo wa kupima “heart rate”.  Daktatri na wauguzi (nurses) walifurahi sana.


Asante sana kwa kusoma makala yangu fupi ya kutembelea  hospitali nyumbani Tanzania

Naitwa Liberatus Mwang’ombe “Libe” kwa 
unyenyekevu wa dhati naomba tushirikiane na unipigie kura

Libe for The DMV Community President 2014
                                


                                

24 comments:

Anonymous said...

libe utaonyesha kila kitu ,atukutaki ,kwa sababu ujatulia bado ,jaribu baada ya miaka mitano.

Anonymous said...

who do u think u fool! Those r just propagandas. We have been there n done that and seen that. I my own opinion I don'tthinku qualified for thay

Anonymous said...

Ni sawa kabisa charity starts from home. Currently wengi wapiga kura our home is here in USA. Mbona hukutujuza wana DMV wenzako about this discussion knowing kuna wavutaji wengi katika jamii yetu hapa DMV?? Kama Nurse Wangu alivyofanya ameorganize medical screeing for free for DMV. Kama wengi walivyosema YOU NEED TO CONNECT WITH THE COMMUNITY UNAYOISHI MORE THAN 75% OF YOUR TIME AND THEN LET US TAKE IT BACK HOME. Inaonyesha ni sera za kujiandaa kugombea ubunge. TUNATAFUTA RAIS WA DMV WHO IS PRACTICAL IN HIS WORDS...
Fundraising ya Eric umekuja na kuondoka was not even interested kusubiri na kujua kuwa kaka yetu kapata nini na what else to do..

Anonymous said...

Go Libe mimi nakupa kula yangu. Mwache Yule aoneshe majengo kama kayajenga kwa pesa zake. Wakati wewe unatoa kwa pesa zako za mfukoni mwako. Wewe ni kiongozi wa ukweli from your articles on your facebook to your contributions to the society.

Anonymous said...

Mbona wanaume wa kimasai na kizulu wanavaa eleni wanakusakama tu. Alafu DJ Lukas unapendelea comment zingine hazina matusi za libe tunaweka ku mtetea huziweki nyingi ni za kumponda unadhani hatuambiani? Tunalijuwa Ilo ukweli utajurikana siku ya kupiga kura na hii isome alafu futika tupa kwenye trash.

Anonymous said...

Kaka Libe,nakushauri uende kugombea uongozi bongo kwani malengo yako ni kusaidia nyumbani. DMV unaweza kutoa changamoto kama mwanakamati+mwanachama,sio lazima uwe Rais ndio tuanze kujua mchango wako. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayofanya nyumbani na huko ndiko wanakuhitaji

Anonymous said...

Charity starts at home! Very true Mr. LIBE BUT I THINK YOU ARE MISSING THE WHOLE IDEA OF A DMV community in the U.S !! Let me give you a little lecture. .DMV community is to bring together all Tanzanian's who are in the DMV area ..that's the 1 and only reason why it was formed and so as to other foreign communities here in the US!! Once we are together then we can look to where and how we can help each other if necessary..We are not a community that is intended to raise funds for Hospitals and schools in Tanzania. ..i salute you and everybody else that is giving back to his/her community back home but lets be honest ..The only reason that we are here its because we saw something was missing in our home country and each and everyone of us knows what was and is still missing there..we are giving back one way or another. ..if giving back home is the reason why we should elect you I don't think you are going to win!! There is a huge amount of Tanzanian's that have been giving back both economical, technological and educational assistance before you Mr LIBE. ...tell us what you have for us ..Tanzania is all ours !! We all love and give back ...even a $50 that is sent home today that is giving back..Tell us what is it that you have for us..

Anonymous said...

This is the tight man! Speaking and conducting himself from the heart.

Anonymous said...

Kweli kijana amepoteza focus,hayo mambo ni mazuri kusaidia nyumbani na wengi wetu tunafanya lakini hatupigi picha kama wewe. Hii sio siasa kijana mdogo. Kama unataka kugombea udiwani huku kwenu Muhumbira Chimara ndio uwapeleke hii article. Mambo ya kijijini kwenu chimara hayatuhusu hapa DMV. Tuambie umeifanyia nini community yetu ya DMV zaidi ya kuwatukana wanawake. Acha propaganda zisizokuwa na msingi wowote. Kama una busara omba msamaha kwanza kwa matusi unayotukkana watu wewe pamoja na timu yako ya kampeni. Dj usiibanie hii ni kuelimisha tu.

Anonymous said...

sasa unagombea ubunge wa kelya au uraisi wa DMV! maana sioni hata picha moja inayoonyesha uliwasaidia vipi watu wa DMV

Anonymous said...

Sasa huyu jamaa angombea uraisi wa Bongo au DMV?, hebu tueleze ulichofanya hapa DMV. I tell you folks, this is a leading indicator that this dude, is after something beyond being DMV president. The DMV president goal is just a stepping stone ili aweze kuuza sura vizuri ubalozini na Bongo.

Anonymous said...

DMV how deep do you believe?
Will you bite the hand that feeds?
Will you bite the hand that gives?
Will you deny the spirit that think abt others?
Will you deny the spirit that unite?
Will you deny the spirit that promotes growth?
Will you deny the spirit that promotes love and happiness?
Do you believe in change?
DMVans, get up off your knees and register to vote.
Are you brave enough to see? Get up of your knees and register to vote.

VOTE FOR LIBE, VOTE FOR CHANGE!!!

Register to vote at www.watanzaniadmv.org

baraka daudi said...

Ndugu Liberatus Mwang'ombe na ndugu Idd Sandaly pamoja na wagombea wengine kwanza nawapongezeeni sana kwa uamuzi wenu wa kugombea nafasi ya kuongoza jumuiya yetu. Tafadhali kamati ya uchaguzi waandae mdahalo ili wagombea wajinadi ili wapiga kura tujue wagombea na tuweze kupiga kura.

Anonymous said...

SISI WATU WA MIKOWANI MSIFANYE MAKO KABISA USHILIKIANO WETU UMEKUFA KWA SABABU YA UYO KIONGOZI WENU IDDI TULIKUWA TUNAPATI KILA MWAKA PAMOJA DMV SASA AKUNA TENA LIBE KIONGOZI MZULI SANA SISI KILA PATI ZETU ZA MICHEZO UWA TUNAMUONA LIBE NA DJ LUKE NA GALAMA ZOTE UWA LIBE NA DJ LUKA NDIO WANANGALAMIA SASA UYO DR LEMI WA NINI ATA HAFAAMU UMUIMU WA KUUNGANISHA WATANZANIA WOTE WA APA USA

Anonymous said...

Myself am not living in USA but I don't understand the dude(Liberatus)all the people,groups and hospitals are in Tanzania.What is his contributions to the DMV Community were he want to be a president?or may be I don't understand.Ndugu unagombea kuwa Rais wa sana DMV na si kwamba unagombea Tanzania.Maana hakuna hata picha moja au tamko lako ulipotoa kauli yoyote kuonyesha unamsaada na community ya wana DMV.

Anonymous said...

GREETINGS KAKA LIBE,TAFADHALI REKEBISHA JINA LA HUYO DAKTARI MWANAUME HALIANDIKWI HIVYO PIA FAHAMU KUWA HUYO MKE WAKE NI DAKTARI BINGWA WA KINA MAMA OBGYN SIYO NURSE KAMA ULIVYOSEMA,NI HIVYO TU,GOOD LUCK

Anonymous said...

Kwani Sandaly alivo anza alionesha nini? This time ana chakuonesha sababu alishakuwa rais akafanya mambo yake ingawa ana dhambi zake kibaoooo ngojeeni siku ya debate mtajurishwa nyie mnaoabudu mapilau na maubwabwa kisa libe kaja kwenye pilau chache mnasema hatumuoni. Na kazi box hangemwachia nani mbona Sandaly alikuwa ajurikani.

Libe hana shida ya kupiga picture ubalozini, Mnadhani huyo mwenzenu. Libe akitaka kwenda ubalozini anaenda any time kwa tkt Yake ya katibu wa DMV wa CHADEMA au kwaajili ubalozi unapendelea CCM tu! Sababu CHADEMA huwa hatuwaoni tunawaona kina Sebo na wenzake tu.
Libe jina lake lipo tayari kwenye list ya waheshimiwa wa DMV. So msimfanye aonekane yuko desparate saaaaana na uongozi. He just wants to try another position and to prove you guys wrong. And to bring change. Muhulizeni Idd ana wanachama wangapi waliojisajiri DMV na wanatoa Ada ? Yeye Si rais mbona anao 20 tu wakati DMV Ina Watanzania zaidi ya 1000. Open your eyes

Anonymous said...

MTI WENYE MATUNDA HUTUPIWA MAWE.

LIBE KAZA BUTI.

MWENDO MKIBUYU.

Anonymous said...

Lakini andika kiswahili lugha ya kizungu naona inawalakini kwako

Anonymous said...

UKWELI NI KWAMBA TUNAHITAJI NGUVU MPYA NA KASI MPYA. SANDALI MZITO SANA MAENEO MENGI LAKINI SHARP SANA KWENDA UBALOZINI WATU AMBAO UBAGUZI. WANYONGE WAKIWA NA SHIDA UBALOZI HAWAONEKANI, WENYE MAJINA MAKUBWA WAKIPATA SHIDA SANDALI WA KWANZA NA UBALOZI WA PILI. THIS TIME WE NEED FIELD MAN, NOT SHOW MAN. KABLA YA MTANANGE MDAHALO UWEPO SAFI.

Anonymous said...

kuwa raisi DMV ni shughuli pevu jamani uwiii! by the time campaign na uchaguzi umeisha raisi anakuwa so exhausted na depressed kutokana na matusi na midomo ya wanajumuiya. anakuwa anahitaji post-election psychological counseling sessions!

Anonymous said...

Mmmhh! Naomba jina la mwalimu wako wa kiswahili,maana sikuelewi kabisaaa!!!!

Anonymous said...

DMV tunayo changamoto this time! Kwa maoni yangu, ni bora kuchagua kiongozi radical ilimradi ana tija kuliko kuchagua kiongozi "Yes sir" asiyekuwa na tija yoyote. Radical anaweza kuwa moderated na kuweza kuongoza kwa mafanikio, lakini kiongozi asiyekuwa na tija ni mzigo.

Anonymous said...

Swali kwa tume ya uchaguzi,tunawaomba wabadili tarehe ya uchaguzi iwe baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Nimeaandaa party ya ushindi,so siwezi kufanya kama ni kipindi hicho. PLEASE PLEASE POSTPONE TO AUG. 8 weekend