ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 9, 2014

Mgomo mpya watatiza Dimba la Brazil


wengi wa wasafiri hulalamikia msongamano na gharama za juu za usafiri nchini Brazil.
Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa mda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya leba nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.

Koti ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya

wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.
Maandamano mengi yamekuwa yakulalamikia hali ngumu ya usafiri lakini sasa wafanyikazi wa treni za mijini ziitwazo Metro ndio waliogoma kutaka nyongeza ya mishahara.
Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo.
Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo?
Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

No comments: