Kwa ufupi
Zilikuwa dakika 10 ngumu kwa mama huyo, Modesta
Simon kuamini hali aliyomkuta mwanaye aliyelazwa hospitali hapo kuuguza
majeraha kutokana na kufanyiwa ukatili na tajiri yake Amina Maige.
Dar es Salaam. Kelele za vilio
jana zilisimamisha kwa muda shughuli katika Wodi ya Wanawake ya
Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam baada ya mama mzazi wa
msichana, Yusta Lucas (20) anayedaiwa kuteswa kwa kung’atwa na kuchomwa
kwa pasi mwili mzima kumwona mwanawe kwa mara ya kwanza.
Zilikuwa dakika 10 ngumu kwa mama huyo, Modesta Simon kuamini hali aliyomkuta mwanaye aliyelazwa hospitali hapo kuuguza majeraha kutokana na kufanyiwa ukatili na tajiri yake Amina Maige.
Mwanamke huyo anashikiliwa katika Kituo cha
polisi Oysterbay kwa tuhumu hizo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Thobias Edoyeka alisema leo atafikishwa mahakamani... “Bado sijafahamu kama atapelekwa ama Kisutu au Kinondoni.”
Mara baada ya mama huyo kuingia katika wodi hiyo, Yusta aliyekuwa ameketi kitandani aliruka na kumkimbilia mlangoni na kilichofuata ni vilio.
Akizungumza huku akitokwa na machozi, Modesta alisema: “Jamani Amina kweli amekufanya hivi, kila nikiuliza wananiambia hujambo kumbe umeharibika hivi...”
Alisema habari za mateso na kulazwa kwa mwanaye alizipata kutoka kwa ndugu yake anayeishi Arusha...
“Alhamisi nilipata simu kutoa kwa ndugu yangu Marieta Shitindi yeye anakaa Arusha, akaniambia ameona kwenye Mwananchi na runinga kwamba Yusta amelazwa baada ya kupigwa na Amina ndipo nikafunga safari kutoka Tabora kuja kuhakikisha.
Amina ni mtoto wa mjomba wangu kabisa na sikuwahi kuambiwa chochote, niliamini wanaishi vizuri na sikudhani kama anaweza kulifanya jambo hili.”
Modesta alisema awali alikuwa na mawasiliano na mwanaye kupitia simu ya mama yake Amina ambaye wanaishi karibu, lakini hivi karibuni alianza kupata wasiwasi baada ya kila alipohitaji kuongea naye alipatiwa sababu hivyo akaomba Yusta kurudishwa na aliahidiwa angepelekwa mwezi huu.
“Aliniahidi mwezi huu atamleta Yusta nyumbani alisema anataka muda amnunulie na cherehani ili akija apate shughuli ya kufanya...” alisema.
Ofisa Muuguzi katika wodi aliyolazwa Yusta, Erica Massawe alisema hali ya binti huyo imeimarika na alisharuhusiwa kutoka tangu Ijumaa iliyopita na kwamba wanasubiri maelekezo ya Polisi na Ustawi wa Jamii kwani ndiyo wahusika wakuu.

1 comment:
Huyo mwajiri ana watoto wake wa kuzaa kweli?? Kina mama kuweni na roho za imani huyu binti ni mtoto wa mtu je what if angekuwa mwanao???? Mama's love is the best, this is the picture of the year hembu angalia alivyomlalia mama yake, you are at peace my dear na mungu atamwangamiza huyo ndugu yako alidhani wewe umekuwa suruali au gauni analopiga pasi!! NYAMAFU
Post a Comment