VIONGOZI WADINI WAKUTANA KUPINGA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
Baraza la viongozi wa dini limekutana Jijini Dar es Salaam kujadili
namna ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya matumizi ya dawa za
kulevya kwa vijana, wanaoendelea kuathirika, pamoja na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na serikali za kukabiliana na usafirishaji,
uingizwaji na matumizi ya dawa hizo.
Tanzania ni kati ya nchi za Afrika zilizoathirika na matumizi na
usafirishaji wa dawa za kulevya, huku Takwimu za Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii zikionyesha kuwa jumla ya watumiaji 20,626 walipatiwa
matibabu katika vituo vya afya kati ya mwaka 2008 hadi 2011.
Takwimu za hivi karibuni za kitengo cha
kupambana na dawa za kulevya cha jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa, tangu mwaka 2010 hadi Mei 2013, jumla ya kilo 742 za heroini, kilo 348 za cocaine, kilo 77 za bangi na kilo 16,335 za mirungi zilikamatwa hapa nchini.
Aidha, tangu July 2013, watanzania 247, wengi wao wakiwa vijana walikamatwa wakisafirisha dawa hizo kwenda nchi za Mauritius, Umoja wa Falme za Kiarabu, China, Pakistan, Brazil na Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa baraza la viongozi wa dini, Alhadi Mussa Salim, anasema viongozi wa dini sasa wameamua kuunganisha nguvu kuwaepusha vijana kuathirika zaidi, na wao wakitumia zaidi nguvu ya vitabu vya imani, kama anavyonukuu moja ya maandiko.
Dkt Harisson Mwakyembe, waziri wa uchukuzi, amefungua semina hii huku akipongeza hatua iliyofikiwa na viongozi hawa ya kutumia nyumba za ibada kupambana na athari za dawa za kulevya.
Na baadhi ya viongozi wa dini wanasema, ni hatua muhimu kwa taasisi za dini sasa kujiingiza kwenye suala hili.
Kwa takwimu za ndani, kati ya kesi 423 za matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya ni kesi moja tu iliyoamuliwa kati ya mwaka 2005 hadi 2013, huku kukiwa na ongezeko la vijana wanaosafirisha dawa hizo kwa matumaini ya kutajirika.

No comments:
Post a Comment