ANGALIA LIVE NEWS
Wednesday, July 9, 2014
KADINDA: NILITAMANI WEMA AWE WANGU
Stori: Mayasa Mariwata wa GPL
MWANAMITINDO maarufu Bongo, Martin Kadinda amesema kabla hajawa kiongozi wake, awali aliwahi kumtamani kimapenzi mcheza filamu Wema Sepetu, lakini alighairi baada ya kugundua ni mwanamke wa kudekadeka.
Kadinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akipiga stori na paparazzi wetu kuhusu masuala mbalimbali yanayomhusu msichana huyo ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz.
Kuhusu maisha wanayoishi nyota hao wawili wapenzi, Kadinda alisema kwa jinsi wanavyoishi ni kama watu wanaoigiza, akitolea mfano wa kipindi walichorudiana wakiwa nchini China, ambako wenyewe walisema wanaigiza filamu wakati ndiyo kwanza walikuwa wanarejesha penzi lao lililovunjika mara ya kwanza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
bado huyu ni manager wake wema?
wivu unamsumbua tu kumwambia mtoto wa watu anadeke deka kwani hajui ndo sifa ya mwanamkee adeke deka na kupetiwa petiwa na mwanamme.mwaaa jamani mijanadume minginewe bwana
Post a Comment