ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 21, 2014

MHE JOSHUA NASSARI KATIKA PROGRAM YA MAFUNZO KWA VIONGOZI WADOGO WALIOONYESHA DIRA MAREKANI

ARUMERU KUANZISHA URAFIKI NA JIMBO LA ARKANSAS
Mbunge wa Arumeru Mashariki, mhe Joshua Nassari amefanya mazungumzo na Seneta Joyce Elliott wa Chama cha Democrat ch Rais Obama Nchini Marekani. Pamoja na mambo mengine wamejadiliana kuhusu mpango wa kuanzisha urafiki kati ya Halmashauri ya Meru na Jimbo la Arkansas la Marekani.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, mhe Joshua Nassari, akitoa mada. Mhe Nassari yupo nchini Marekani Pamoja na vijana wengine toka nchi zote za Afrika kwa ajili ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira (most promising young African leaders) iliyoanzishwa na Rais Obama.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, mhe Joshua Nassari,katika picha ya pamoja na vijana wengine toka nchi zote za Afrika kwa ajili ya program ya mafunzo kwa viongozi wadogo walioonyesha dira (most promising young African leaders) iliyoanzishwa na Rais Obama.

1 comment:

Anonymous said...

lugha, lugha, lugha jamani!!!
Kwa nini tusiwaite "viongozi wanaoibukia" badala ya "viongozi wadogo"?