ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 21, 2014

MAALIM SEIF ATEMBELEA MICHEWENI LEO

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Mzee wa Makangale, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Micheweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji Bi. Habiba Mkadam Hamad wa kijiji cha Makangale baada ya kumjuilia hali, akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Micheweni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika kijiji cha Makangale, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Micheweni. Kijiji cha Makangale ni maarufu sana kwa ulimaji wa viazi vitamu kama vinavyoonekana katika picha.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Micheweni, wakati akiwa katika ziara ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Micheweni.
Wanawake wa Micheweni wakiwa na shauku ya kutaka kumsalimu Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea kijijini kwao kuangalia wagonjwa. (Picha na Salmin Said, OMKR)

No comments: