Ndugu zetu wana DMV. Kama mnavyomjuwa na kuijuwa timu Iddi (TEAM TANZANIA) kwamba huwa hatupendelei kuingia kwenye malumbano wala kwenye shutuma kwa wagombea wengine. Lakini tumeona kuna haja ya kuweka wazi au kuondoa upotoshaji wa Liberatus Mwangombe anao wafanya ninyi wana DMV, Watanzania na Wanadiaspora.
Timu Iddi Sandaly, inapend kufafanua maswala haya Matatu:
KUGHAIRISHWA KWA UCHAGUZI.
HARASSMENT ANAYODAI KAFANYIWA LIBERATUS NA VIONGOZI PAMOJA NA ASHA NYANGANYI.
Tunadhani ni kipindi cha Kaka Liberatus Kutambua kwamba DMV kwanza na Aache upotoshaji wa Hali ya Juu.
Hatotozungumzia kuhusu kikao kizima na Muheshimiwa Balozi kwani kiongozi Bora ni yule anaeweka Mijadala inayofanyika ya kuendeleza jumuiya mbele kuliko kuweka matashi na maslahi binafsi. Timu yetu inamuheshimu Balozi na Tunampongeza kwa kazi nzuri na maamuzi mazuri aliyoyafanya ili kuweza kuijenga jumuiya yetu.
Ki ufupi Maamuzi yote yaliyofikia kwenye kikao hicho yalikubaliwa na Wagombea Wote, Tume ya Uchaguzi, Bodi ya wakurugenzi ya Jumuiya na Muheshimiwa Balozi. Mkutano uliwashirikisha watu kama 20. Tunamshukuru Balozi na Maafisa wa Ubalozi kwa Kutumia Muda wao ilikusimamisha Jumuiya Yetu.
Timu Iddi Sandaly, inapend kufafanua maswala haya Matatu:
KUGHAIRISHWA KWA UCHAGUZI.
Uchaguzi uligharishwa kutoka June 20 kwenda July 21, kwa sababu wagombea wengi hawakuqualify kugombea kwa vile hawakuwa wanachama. Ndugu Liberatus Mwangiombe Almejiunga na Jumuiya tarehe 3, Mwezi wa Sita tu (June 3, 2014) , ili agombee na hakuwa mwanachama hai kabla ya hapo. Ni Iddi Sandaly na wagombea wengine wawili tu ndio walikuwa wana sifa za kugombea. Lakini tume ilionea kuna haja ya kuwa na uchaguzi wenye kuleta Muamko na Sababu nyingine za Tume. Mgombea Iddi Sandaly hakuwa mchoyo akalikubali hili. Katiba inasema:
ELIGIBILITY
Only paid active members are
eligible to run for any office of the Association. All membership dues shall be paid at least 30
days prior to the election date to be eligible for nomination. A list of paid financial members shall be
made available by the Treasurer for the purpose of election.
Only active members who have
resided continuously for a minimum of two years in the METRO, immediately prior
to the election date may contest for the office of the president.
Tarehe Ilibadilishwa Tena na tume kwa Sababu ambazo Tume iliziona ni Sababu endelevu kutoka July 21, kwenda August 9.
Picha Ya Pamoja Baada Ya Kikao. Liberatus Akiwa na Tabasamu karibu na Mh. Balozi.
HARASSMENT ANAYODAI KAFANYIWA LIBERATUS NA VIONGOZI PAMOJA NA ASHA NYANGANYI.
Ni kwamba baada ya
Liberatus kutoa video ya kampeni ya na kulishambulia Darasa la kiswahili. Asha Nyanganyi kama Mmoja wa Waanzilishi, Msemaji mkuu na Mwalimu wa Darasa la Kiswahili aliwasiliana na Liberatus na Viongozi kwenye email zifuatazo. Naomba mzisome kwa makini. Iddi Sandaly Aliandika response moja TU. Na Ray makamu wa Rais aliandika email mbili Tu. Zote zime ambatanishwa hapa. Hakukuwa na Harassment.
Liberatus kutoa video ya kampeni ya na kulishambulia Darasa la kiswahili. Asha Nyanganyi kama Mmoja wa Waanzilishi, Msemaji mkuu na Mwalimu wa Darasa la Kiswahili aliwasiliana na Liberatus na Viongozi kwenye email zifuatazo. Naomba mzisome kwa makini. Iddi Sandaly Aliandika response moja TU. Na Ray makamu wa Rais aliandika email mbili Tu. Zote zime ambatanishwa hapa. Hakukuwa na Harassment.
Tunadhani ni kipindi cha Kaka Liberatus Kutambua kwamba DMV kwanza na Aache upotoshaji wa Hali ya Juu.
KUHUSU IDDI KUTOA AMRI KWA KAMATI.
Liberatus amepotosha kwa kuweka text mbili tu . Mawasiliano hayo yalifanywa kwenye TZ Diaspora DMV group ambayo ina watu 50, Wakiwemo wajumbe wote wa kamati ya Uchaguzi na Mwenyekiti wa Tume, na vile vile akiwemo Election Strategist wa Liberatus ALAWI kama Mnavyoona hapo chini kwenye hii image. Hii Haikuwa message kati ya Iddi na Asha.
Mjadala ulikuwa kati ya Iddi Sandaly na Liberatus lakini Solomon YEYE akiwa ni mgombea vile vile alianza kwa kuungana na Libe na Kuingilia kati mjadala uliokuwa unaendelea kati ya Iddi na Libe. Hii ilisababiswa kwa Vile Solomon alijiona hana mpinzani na akamua kuambatana na Liberatus ili kuweza kumuangamiza Iddi. Kutoka na Hali hii Ndipo bwana iddi Aliandika haya hapa chini. Tunaomba Muelewe kuwa hii Haikuwa Direct Text/Private Text ya Kutoka kwa Iddi kwenda kwa Asha.
Mwisho tunaomba Liberatus Mwangombe aache Tabia ya Kuwashambulia kila mtu, Aache kushambulia watu wanaomuunga mkono Ndugu Iddi, Ache kuishambulia Tume ya Uchaguzi, Ache kuishambulia Bodi ya Jumuiya, Aache kuushambulia uongozi unaomaliza muda wake na Aache Kuushambulia Ubalozi na Muheshimiwa Balozi.
TIMU IDDI
DMV KWANZA