ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 9, 2014

MTOTO WA MIAKA 9 AVUNJA RECORD YA KUFIKA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO


Mtoto Idda Baita ni mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi ya uwanja wa ndege moshi amevunja record ya kuwa mtoto wa kwanza wa kike kufika kilele cha Mt Kilimanjaro chenye urefu wa M. 5739. Hapa unaweza kuona Idda ni kiasi gani ana sikia baridi na pia kujisikia mshindi kwa kuinua mikono juu kwa furaha ya kufika kileleni hapo.
 Idda alitumia njia ya Umbwe, Kibosho njia inayosemekana kuwa ni ngumu hata watu wazima utokwa makamasi na jasho kuwakauka watumiapo njia hii kuelekea kilele cha Mt Kilimanjaro. Idda amesema atakuwa balozi mzuri wa Kilimanjaro National Park kwa watalii wanaokuja Tanzania kwa madhumuni ya kupanda Mt Kilimanjaro.

No comments: