Waziri mkuu wa Australia, Tony Abbott, anasema kuwa hakuna usimamizi mzuri katika eneo ambapo ndege ya Malaysia ilianguka wiki iliyopita.
Anasema huenda ni kwa hakika wapiganaji wanaoiunga Urusi mkono waliidunguwa ndege hiyo na jinsi wanavyolidhibiti eneo hilo ni kama kuwa na wahalifu wanaosimamia eneo ambalo uhalifu umefanyika.
Raia 37 wa Ukraine walikuwa miongoni mwa watu 300 waliouawa.
Australia inaunga mkono azimio la Umoja wa mataifa la kutaka wachunguzi waruhusiwe kuingia katika eneo hilo kufanya uchunguzi wa kina.
Haya yakijiri, Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema kua atafanya kila awezalo, kuhakikisha kuwa mgogoro wa Ukraine unapata ufumbuzi
Rais Putin alitoa taarifa mapema asubuhi ya leo ambalo lilionekana kwenye mtandao wa ikulu ya Rais.
Tangazo lenyewe ni kinyume na matamshi aliyotaoa wiki jana aliposema kuwa maafisa wa Ukraine ndio wa kulaumiwa kwa kutokea kwa ajali hiyo.
Putin amesema kuwa tukio hilo linapaswa kuungunisha mataifa hayo mawili wala sio kuleta mgawanyiko zaidi ingawa aliongeza kwamba kama makubaliano ya kusitisha vita Ukraine Mashariki yasingevunjika mwezi Juni na mapigano kuanza tena, mkasa huu umgezulika.
Alisema kuwa kila mtu katika eneo hilo ambaye amehusika katika mgogoro huo anapaswa kuwajibika.
Alisema ni muhimu kufanya kila liwezekanalo, kuhakikisha usalama wa wataamu wa kimataifa katika eneo hilo unahakikishwa, ili wataalamu hao waweze kufanya uchunguzi.
Pia ametoa wito wa kuruhusu misaada kuweza kuwafikia waathiri wa wa vita.
BBC
1 comment:
waongo wa dunia
Post a Comment