Mwenye shati ya mikono mirefu aliye kaa mkurungezi wa halmashauri ya msalala patrick karangwa akiwa na vijana waliomaliza mafunzo ya ufungaji wa sola toka kata 20 za jimbo la msalala wakishirikiana na Rex energy toka dar es saalm mafunzo ya siku mbili
Eng john maijo akitoa maelezo juu kwa fundi mkuu moris mlaponi juu ya kufunga panel za sola juu ya paa la la jengo la shule kwa ajili ya kuanza kazi .
Mkurungezi wa halmashauri ya msalala patrick karangwa akisalimia na vijana walio maliza mafunzo ya ufungaji wa sola .
Mwanafunzi wa shule ya sekondary ya mwalimu nyerere mariamu david akiwa darasani kwa ajili ya kushukuru kampuni ya Rea kwa kuweka umeme wa sola katika shule yao .
Mkurungezi wa msalala patrick karangwa akitoa maelezo kwa vijana kwa kumaliza mafunzo ya ufungaji wa sola kati jimbo la msalala .
Mashine ya kupoza umeme pwm sola charge controller vs 6024n ikiwa tayari kwa kuanza kazi
Mafundi toka Rex jemes kinyo na moris mlaponi wakiwa wamemalinza kazi ya kuweka sola shule ya sekondary ya mwalimu nyerere .
Afisa elimu wa sekondary taalamu elias ghozi akimkaribisha mgeni rasm mkurungezi wa hamashauri ya msalala wakati wa kufungaji wa mafunzo ya kufunga sola.
Mkurungezi wa halshauri ya msalala patrick karangwa akisalimia na baadhi ya vijana waliomaliza mafunzo ya sola baada ya kumaliza mafunzo ya siku saba
Wanafunzi wa shule ya mwalimu nyerere wakisikiliza hotuba ya mbuge wa jimbo la msalala ezekiel maige hayupo picha kwa shukurani ya kuwekewa sola katika shule yao .
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondary ya mwalimu nyerere peter kweba mwenye suruali ya kaki akisalimia na ugeni wa msafala wa mbuge wa jimbo la msalala ezekiel maige
Mwalimu peter kweba anacheka akiwa na mbuge wa jimbo la msalala ezekiel maige kati na kulia ni afisa elimu taaluma ntobi ghozi wakienda kukangua huwekaji wa umeme wa jua katika shulle ya sekondari ya mwalimu nyerere .
Mafundi wakiendelea na kazi ya kufungaji wa vifaa ya vya sola .
Mafundi wakiendelea na kazi ya kufungaji wa sola
Eng john maijo na fundi mkuu moris mlaponi wakiweka pannel za sola juu ya paa .
fundi mkuu moris mlaponi ambaye ameshika pannel ya sola kwa ajili ya kufunga juu ya paa la shule .
Makamu wa shule ya sekondari ya mwalimu nyerere john machela mwenye suruali nyeupe na afisa elimu taaluma ntobi ghozi wakibadilishana mawanzo juu ya kupata umeme wa juu katika shule yao .
Baadhi ya pannel za sola juu ya paa zikiwa tayari juu ya paa kwa ajili ya kazi .
Mafundi wakiendela na kazi zao .
Mbuge wa jimbo la msalala ezekiel maige aliyeyoosha mkono akitoa maelezo juu ya kutunza mali hiyo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo juu ya ulinzi wa sola hizo .
Mbuge wa jimbo la msalala ezekiel maige akiongea na wanafunzi wa shule hiyo juu ya kutunza vifaa hiyo
fundi akijalibu kuweka kifaa chaki vizuri
Mbunge wa jimbo la msalala akisisitiza jambo juu shule kumi na sita za sekondari kupata huduma ya sola katika shule za jimbo la msalala .
Afisa elimu taalum ntobi ghozi akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya mwalimu nyerere .
Mafundi wakiwa juu ya dali kwa ajili ya kufungaji wa wanya juu .
Baadhi ya betry za sola zikiwa tayari kwa kazi .
vijana wakichimba mfereji wa kupitisha wanya chini ya ardhi katika shule ya sekondari ya mwalimu nyerere toka juu kwenda chini
Na Mohab Dominick
Kahama
Julay 21, 2014.
MBUNGE wa Jimbo la Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Ezekieli Maige amesema kuwa hadi kufikia mwezi Septemba mwaka huu hakutakuwa na shule yeyote ya sekondari ambayo haitakuwa haina umeme katika jimb o lake.
Maige aliyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa umeme wa mionzi ya jua katika Shule ya sekondari ya Mwalimu Nyerere iliyopo katika jimbo la Msalala ikiwa ni moja kati ya shule 20 zilizopo katika jimbo hilo zinazotarajiwa kupata umeme wa mionzi ya jua kwa kufadhili wa Wakala wa umeme vijijini (REA).
Maige alisema kuwa umeme huo umekuja kwa awamu ya nne katika shule hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa hazina umeme hali ambayo ilifanya Wanafunzi kusoma katika mazingira magumu na kuchangia kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho.
Alisema kuwa ameamua kutumia kampuni ya Rex Enegy ambayo ndio inafunga umeme huo katika shule hizo chini ya usimamizi wa Wakala wa umeme Vijijini hali ambayo inatarajia kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu katika jimbo hilo.
Maige alisema kuwa kwa kutumia umeme wa Shirika la umeme Tanzania Wazazi hawawezi kumudu kuchangia gharama za uendeshaji (Bill) hali ambayo inaweza kufanya shule hizo kukatiwa umeme mara kwa mara kutokana na kutomudu gharama hizo.
Mbunge huyo alisema kuwa mradi huo umepatikana kutokana na kuandika maombi mara kwa mara na kuzingatia kuwa Wilaya ya Kahama inaongoza kwa wimbi la Wanafunzi wa kike wa shule za sekondari kupata mimba Mkoani Shinyanga.
Pia Mbunge huyo aliwataka Wanafunzi wa shule hiyo ya Mwalimu Nyerere pamoja na nyingine kuhakikisha kuwa wanatunza miundombinu ya mradi huo uli uwe wa kudumu na wanafunzi waweze kufaidika hasa wakati wa kujisomea usiku.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Mwalimu Nyerere Peter Kweba alishukuru kwa kupata mradi huo na kuongeza kuwa kwa sasa Wanafunzi wataondokana na matatizo ya kusomea mishumaa pamoja vibatari vilivyokuwa vikiwaathiri kiafya.
Kweba alisema kuwa hata Walimu sasa watapata fursa ya kufanya shughuli zao kama za kuchapisha mitihani hapo hapo shuleni badala ya kutumia kiasi cha shilingi milini moja na nusu walizokuwa wakitumia katika kuchapisha mitihani nje ya shule.
Picha na habari na Mohab Matukio Blog
No comments:
Post a Comment