ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 19, 2014

BARAZA LA MADIWANI CHATO LATOA TUZO ZA ELIMU

Bi. Leticia Pastory wa Kadama English medium akipokea ngao na cheti kwa kuwa mshindi wa kwanza katika mtihani wa darasa la saba wilayani Chato.
Bw. Edward Leornad mratibu wa elimu kata ya Kasenga akipokea cheti cha kata ya kwanza kiwilaya katika mtihani wa darasa la saba 2013
Bw. Lucas Nicholaus mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Kamanga shule iliyokuwa ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba 2013 akipokea kinyago, ambacho hukabidhiwa kwa shule inayofanya vibaya kila mwaka
Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika kikao cha robo ya nne

Baraza la madiwani la halimashauri ya wilaya ya chato katika kikao chake robo ya nne, limetunuku vyeti, ngao na pesa Taslimu ikiwa ni pongezi kwa shule na kata zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba 2014.

Shule binafsi zilizoongoza ni shule ya msingi Kadama (Kadama English medium), ikifuatiwa na shule ya msingi Emau ( Emau english medium) zote zipo wilayani Chato.

Shule za serikali zilizoongoza ni shule ya msingi Magiri iliyoshika nafasi ya kwanza, nafasi ya pili ilimeshikwa na shule ya msingi Minkoto “A”, na kufuatiwa na shule ya msingi Imalabupina iliyoshika nafasi ya tatu, huku shule ya msingi Kamanga iliyopo kata ya Makurugusi ikishika nafasi ya mwisho na kukabidhiwa kinyago.

Kata zilizofanya vizuri katika tuzo hizo ni pamoja na Kasenga, Muganza na Buziku.
Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Chato limewatunuku vyeti vya pongezi wananchi wawili wa kata ya Nyamirembe Ndg. Rajabu Athumani Ndugala na Abdu Ibrahimu Mpisi ambao walifanikisha ujenzi wa madarasa mawili na ofisi ya mwalimu shule ya msingi Nyamirembe B kwa gharama ya Tshs.16,000,000, huku halmashauri ya Wilaya ya chato ikikamilisha madarasa na fisi hizo kwa kwa thamani ya Tshs.15,000,000.

Afisa elimu wa wilaya ya Chato Bw. Angasirini Obedi Kweka akitoa maelezo kwa baraza la Madiwani kabla ya kukabidhi tuzo hizo alisema, Ufauru mzuri wa wanafunzi huchangiwa na uwepo wa walimu wakutosha na wenye kuwajibika, chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni na ushirikiano baina ya wanajamii.

Bw. Kweka aliendelea kuelezea changamoto zilizopo mashuleni, hususa ni madawati ambayo yamekuwa changamoto kubwa hasa shule za msingi ambapo alisema idadi ya wanafunzi inazidi kuwa kubwa ukilinganisha na idadi ya madawati yaliyopo , hivyo aliliomba baraza la madiwani kulifanyia kazi tatizo hili

No comments: