Shilole akiwa na Nuh Mziwanda enzi za mapenzi motomoto!
Stori ya Nuh Mziwanda kujichora tatoo yenye jina la Shilole ilisambaa sana na wengi walikua wakijiuliza siku ikitokea wameachana itakuaje hasa upande wa Nuh ambaye ndiye aliyejichora tatoo hiyo.
Maelezo ya Nuh Mziwanda yamedai kuwa sababu zilizosababisha waachane ni miss call na msg ambayo aliikuta kwenye simu ya Shilole ambayo inasemekana ilitumwa na mwanaume, akimjulisha kuwa amesha ingia mjini, Nuh alipomwambia Shilole apige alionekana kujikanganya na hapo ndipo mtiti ulivyoonza baada ya Nuh kumpiga kibao mpenzi wake huyo ndiyo moto ukawakia hapo.
2 comments:
Waswahili wanasema "Usipande mbuyu ukadondosha ngazi".Ngoja tuone atashuka vipi..
pole ndugu yangu Nuh unafikiri wewe unauwezo wakutunza dada kama huyo?wako wazee watunzao wewe umependwa kwa uhandsome wako...kubali yaishe hunahaja ya kumpiga vumilia au tafuta mwingine basi
Post a Comment