Chris mwenye umri wa miaka 9 akiwa na dada yake kabla ya kapoteana wakiwa njiani kuelekea New York Central Park Zoo E 64th St. Chris alijikuta yupo maeneo ya Port Authority Bus Terminal ndipo alipojisalimisha mikononi mwa polisi na kusema kuwa amepoteana na wazazi wake ambao hata kuongea kiingereza hawajui wakiwa Central Park Zoo wakishangaa wanyama. Chris alipoteana na wazazi wake kuanzania saa 10 jioni hadi saa 12:30 jioni ndipo alivyojisalimisha mikononi mwa NYPD wamsaidia kuwatafuta wazazi wake.
Chris alijikuta amesha poteana nao kabla ya kufika hapa Central Park Zoo, Zoo hii ni maarufu na wanyama wanaopatikana hapa ni Mbuzi, Kondoo, Sungura Pia kuna kuku na bata.
Chris alipatika mitaa 20 kutoka Central Park Zoo wazazi wake na mdogo wake walikuwa wakishangaa wanyama na yeye kuanza kukata mitaa. Anasema sababu ya kukata mitaa ni furaha kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika New York City na alijikuta akipoteana na wazazi wake wakati akishangaa vikwangua anga hasa mataa ya Times Square.
No comments:
Post a Comment