ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 19, 2014

MWANAMKE KABLA YA NDOA, ANATAKIWA AWE ‘AMETOKA’ NA WANAUME WANGAPI?


NIswali gumu lakini jepesi kwa mtazamo. Wengi wamekuwa wakiingia katika mjadala huu bila ya kujua suala lenyewe lina sura mbili tofauti.

HAITAKIWI
Kwa majibu ya maandiko matakatifu mwanamke na mwanaume hawana ruhusa ya kukutana kimwili mpaka pale watakapopata baraka halali ya kuishi kama mume na mke. Kwa hiyo kumbe hakutakiwi kuwa na idadi!

Baraka hizi kwa siku hizi zinatoka makanisani (kwa Wakristo), misikitini (kwa Waislamu) na katika ofisi za serikali, wengi huita Bomani na husimamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya. Lakini pia kuna ndoa za kimila ambazo husimamiwa na makatibu tarafa.

NI DHAMBI
Kinyume na hapo, kukutana kimwili au kuzini ni dhambi mbele za Mungu. Wataalam wa maandiko wanaiita dhambi hii ni ‘ya kupanga’ na kuamua tofauti na nyingine kwa hiyo anayeitenda anakusudia.

HAKUNA KIFICHO
Lakini cha ajabu katika zama hizi za utandawazi, suala la wachumba au watu wasio katika ndoa kukutana kimwili limekuwa jambo la kawaida huku wengine wakilifanya halali kwa wazazi au ndugu.

IDADI KUBWA KIELELEZO?
John Tommy mwandishi wa Kitabu cha Love Me, Love You aliwahi kusema kuwa idadi kubwa ya wanaume waliofanya mapenzi na mwanamke mmoja kabla hajaolewa ni kielelezo tosha kwamba, mwanamke huyo hawezi kuja kuwa mwaminifu katika ndoa.

Alisema mwanamke aliyelelewa kimaadili, akakulia katika maadili hayo hadi kuolewa, angalau awe amefanya mapenzi na wanaume watatu, akiwemo anayemuoa. Hii ni taswira ya kuonesha uaminifu katika ndoa halali na kuifanya idumu.

WATU WANASEMAJE?
Baadhi ya watu wazima waliozungumza na safu hii kwa nyakati tofauti walisema, kwa kawaida mwanaume wa kwanza kulala na msichana ambaye hajaingizwa ‘ukubwani’ siye atakayemuoa.

Kwa mujibu wa uzoefu uwezekano wa mwanaume huyo kutooa ni kwa sababu anakuwa mdogo kiumri. Mwanaume atakeyefuata atatenda jambo moja ambalo litamfanya msichana amuone mwongo na hivyo kutengana naye.

Wazoefu hao wanasema mwanaume wa tatu ndiye ambaye ana nafasi kubwa ya kutoa mwanga wa maisha ya ndoa kwa msichana akitangaza uchumba na ahadi nyingine ambazo awali msichana huyo hakuwahi kutamkiwa na waliomtangulia.

Na kipindi hicho ambacho msichana anaweza kuanza kuonekana kama anakomaa kiakili.
“Ukimuona mwanamke mpaka anaolewa ameshalala na wanaume zaidi ya watano hadi sita huyo ana hulka ya umalaya na hatakuwa mwaminifu katika ndoa. Kama una historia ya mwanamke wa sampuli hiyo jaribu kufuatilia nyendo zake,” alisema bibi mmoja anayepata miaka 76 sasa hapa duniani.

Itaendelea wiki ijayo.
GPL

No comments: