ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 4, 2014

NAKUJA KUMTEKETEZA SHILOLE

MKALI wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade amesema yupo tayari kuja kumteketeza mkali wa miondoko ya mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Agosti 8, katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mkali wa muziki kutoka pande za Nigeria, Yemi Alade.
Akizungumza na Over The Weekend, kwa njia ya simu, Yemi ambaye ametokea kujizolea umaarufu mkubwa kupitia wimbo wa Johnny, alisema kuwa amejipanga vya kutosha na haoni kama kuna mwanamuziki atakayemsumbua hapa Bongo huku akisisitiza anakuja kumteketeza Shilole ambaye aliambiwa kuwa anatisha Bongo.

“Tanzania ni nchi nzuri najua na wanamuziki wake wapo vizuri, nimeambiwa kuna mwanamuziki anaitwa Shilole mwambieni tu nakuja kumteketeza na shoo zangu huwa hazina mpinzani.
“Nitafanya shoo ya mwaka ya kihistoria siku hiyo na lazima nimchukue Johnny wangu uwanjani hapo na kurudi naye kwetu Nigeria,” alisema Yemi.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Yemi anatarajiwa kushuka Dar kesho Jumanne saa tano kamili usiku na Shirika la Ndege la Kenya Airways, tayari kwa kupiga shoo ya kufa mtu ambapo ataungana na wakali kutoka Bongo kama Ali Kiba, Shilole, R.O.M.A, Meninah, Navy Kenzo, Nyandu Toz, P-Plan, Juma Nature na kundi zima la TMK Wanaume Halisi pamoja na Rais wa Manzese, Madee.
Pia kutakuwa na burudani tofauti katika tamasha hilo ambazo ni ndondi, mechi kali kati ya timu ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar FC, Wabunge Mashabiki wa Simba dhidi ya Yanga, Bongo Fleva dhidi ya Bongo Movie na Wanamuziki wa Injili.

No comments: