Advertisements

Sunday, August 10, 2014

TAMKO: TEAM LIBE FOR DMV COMMUNITY PRESIDENT 2014 JUU YA UCHAGUZI

Mgombea Urais Libe akiwa na dada yake na Eric wakati uchaguzi ukiendelea.

Baada ya muda wa ukumbi kuisha na kura zikiendelea kuhesabiwa: matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;

Urais
Idd Sandaly kura 231
Liberatus Mwangombe Kura 214
Jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430
Hii inamaanisha Idd amepata 53.7% ya kura zilizo pigwa na Liberatus amepata 49.76% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia, unapata 107.89%. Swali; 7.89% imetoka wapi?

Ukijumlisha kura za Idd na Liberatus 231 +214= 445.  Hii inaonyesha tofauti ya kura 15 huku Idd akiongoza kwa kura 17. Hii inamaanisha kulikuwa na kura za ziada 15, yani kura 15 zilikuwa hazijulikani zilipo toka. 

Wakala wa Liberatus alipewa kura 8 za absentee ballots na wakala wa Idd alipewa kura 4 za absentee ballots.  Tatizo hapa; hatukupewa idada ya watu walio piga absentee ballot na wala hawakusema ni ngapi zimeharibika.

Ukijumrisha kura za ukumbini na absent ballot, matokeao ni;
Idd Sandally 231+4= 235
Liberatus Mwangombe 214+8= 222
Hii inaonyesha Idd anaongoza kwa kura 14

Swali kuu ni kuwa; Zile kura 15 zilizo zidi zime tokea wapi?

Baada ya kuona mapungufu haya kwenye kura; Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Ndg. Safari alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi kutangaza mshindi; lakini atatangaza numbers. ALITANGAZA NUMBERS ZA UWANJANI TU, HAKUTANGAZA ABSENT BALLOT.  Wakati sintofahamu hili likienedelea; “Team Libe for DMV Community President” iliomba “re-count”; ikashindikana kufanya re-count baada ya polis kuchukua mic na kufukuza kila mtu ukumbini.  Watu wote walitoka ukumbini ndani ya dakika moja.  Ikumbukwe; ukumbi ulichukuliwa hadi saa nne usiku.  Wakati tunafukuzwa na polis ilikuwa ni saa tano usiku.  Mwenyekiti wa Board Ndg. Hamza Mwamoyo aliondoka na kura zote akidai tutafanya re-count.

Kipengele kingine ambacho kilikuwa na utata ni cha makamu wa Rais. Ieleweke kuwa; box la makamo wa rais na Rais lilikuwa moja. 

Nafasi ya makamu wa Rais matokeo yalikuwa kama ifuatavyo;
Heriet Shangarai kura 333
Salma Moshi kura 94
Ukijumrisha matokeo ya makamu wa raisi unapata jumla ya kura 429.  Hii bado inaonyesha ukakasi; kwa nini kura za Rais ziwe jumla 445 na makamu 429 na zote zimetoka kwenye box moja; na karatasi linalo tumika kupigia kura lina katwa sehemu mbili, ya juu ni ya Rais na chini ya Makamu wa rais; zote zinaingia kwenye box moja.  Hoja; kwa nini number za makamu wa Rais na Rais don’t add up! Au, kwa nini number za mgombea wa makamu wa mwenyekiti  zime “match” na wapiga kura; wakati number za raisi hazijamach na zote zinatokea wenye box moja (zinatofauti ya kura 16)?

Itambulike kuwa; msimamo wa “Team Libe for DMV Community President 2014” unaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua mgogoro huu ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko.  Pia, wahusika watambue kuwa; Liberatus ana watu zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambayo ni  walio mpigia kura ambao wanahitaji kupewa majibu stahiki.  Ustawi wa jumuia upo mikonpni mwa Tume ya Uchaguzi.   Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president wawe na uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.

Imetolewa August 9, 2014
Mwanaid Love “Mona”/ Campaign Manager

UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL

7 comments:

Anonymous said...

Hapa pana kamchezo kamefanyika hapa uchaguzi na urudiwe tafadhali na this time mufanye na debate kabla ya uchaguzi kurudiwa.

Anonymous said...

We move forward,viongozi ni hawa, Rais Iddi, Makamu Rais Harriet, Katibu Saidi, Naibu Katibu Bernadetta, Mweka Hazina Jasmine. Habari ndio hiyo!!!Next!!

Anonymous said...

Kura zihesabiwe na watu kutoka majimbo tofauti.Waombwe watu kutoka NY au Connecticut ambao hawana support kwa Iddi au Libe. Maana yangu ni watu ambao ni independent. Hii itasaidia kutatua tatizo la either conflict au appearance ya conflict of interest.

This is so embarassing. Tunashindwa kuhesabu kura 450, je ingukuwa kura 1,000 au 100,000 au 1,000,000?.

Anonymous said...

Number zako haziko sawa kama maandishi yako yalivyokuwa hayako sawa,chamsingi kubali matokeo,kwa kawaida mshindi siku zote ni mmoja,wewe ndio unaanza kuwatengenga wana watu.tunataka kusonga mbele sio kulalamika haitasaidia kitu chochote.chamsingi ni kutazama ya mbele tena.tusubiri uchaguzi mwingine tena ,huu ushapita.
Pole dada.

Anonymous said...

Jamani tendeni haki hata kwa Mwenyezi Mungu. Ukiangalia hizo numbers sipati picha. Huu uchaguzi ni batili.

Anonymous said...

LIBE Sina Shaka UBUNGE 2015 hauta kosa. Ni believe you learned a lot from this campaign. Do take it as a challenge and go back home campaign for MP position. Mungu kakupangia makubwa zaidi Mbele yako. All the best.

Anonymous said...

Baada ya wizi mchana kweupe, mnatuambia Move forward?, kwanini mlileta uchaguzi kama mlikuwa na mtu wenu wa kubandikiza?. tutawachia jumuia yenu muendelee kupeana