ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 22, 2014

MH. PINDA AHUDHURI IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MWAIPOPO WA DAYOSISI YA SUMBAWANGA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto) katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo katika Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakiwa katika Picha ya pamoja na Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo na mkewe Tunsume Mwaipopo (kulia) katika ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

No comments: