Wednesday, October 22, 2014

Katiba mpya itatowesha madhila ya sheria kandamizi ya ndoa ya mwaka 1971: Dk Chana

Wakati wa mahojiano Dk. Pindi Chana na Joseph Msami.(Picha ya UM/Idhaa ya kiswaili)

Juhudi za kutokomezwa kwa ndoa na mimba za utotoni huenda ziakatimia nchini Tanzania baada ya kuingizwa kwa kipengele cha kumtambua mtoto kuwa ni mtu yeyote aliyeko chini ya umri wa miaka 18 katika rasimu ya katiba. Amesema naibu waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Dk Pindi Chana.

Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Dk Chana ambaye amehutubia baraza hilo juu ya mafaniko ya Tanzania katika kutokomeza malaria amesema sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ni kikwazo lakini kuna matumaini.Pia amezungumzia mafanikio ya uwezeshaji wa wananwake lakini kwanza anaanza kwa kufafanua suala la sheria kandamizi la ndoa.

KUSIKILIZA BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake