Monday, October 27, 2014

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wakikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo leo Jumatatu Oktoba 27, 2014
:Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na vijana baada ya kutembelea kampuni ya mawasiliano ya VIETTEL Jumatatu Oktoba 27, 2014 Jumatatu Oktoba 27, 2014.

PICHA NA IKULU

2 comments:

Anonymous said...

Asante mhe. Rais wetu! Sasa muda huu uliobakia ulitakiwa kukaa nyumbani na kutafakari yale ulioyowatendea waTanzania na umalize ngwe kwa kutenda kitu muhimu! safari zimezidi ! Hivi jirani yako Mhe. P. Kagame mbona hana safari nyngi hivyo na nchi yake imeboreka sana kwa kwenda mbele!? wametuzidi kabisa. asante.

Mtanzania Mkereketwa said...

Tangu rais wetu awe anasafiri mara kwa mara kuna mafanikio yanayotokana na safari zake, je nani anaweza kunitajia kadhaa ambayo moja kwa moja yanaweza kuhusishwa na safari zake. Nahitaji hili kwa kazi fulani nisaidieni