ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, November 16, 2014

MWANADIASPORA DMV AHUTUBIA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE NA KUWATIA MOYO SIKU 2 KABLA YA MTIHANI WA MWISHO

Akiongea na watahiniwa wa kidato cha nne siku mbili kabla ya mtihani wa Taifa 2014, shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali, Mwana-diaspora na "alumni" wa Montfort kutoka Washington, D. C., Marekani, Liberatus Mwang'ombe "Libe" alianza kwa kusema, Montfort ni shule aliyo soma na anajisikia faraja akiyaona mazingira yale. Aliendelea kwa kusema, maamuzi ya mwisho ya kila binadamu yapo chini ya himaya yake. Alisema "huwezi kutegemea mtu baki au mwingine aongoze au arutubishe maisha yako, ni wewe binafsi unaweza kufanya tofauti kwenye maisha yako na kila binadamu ni kiongozi. Pia alisema anaamini kuwa kila binadamu ana ndoto zake kwenye maisha; alisema; "ni muhimu kujiwekea malengo ya ndoto zenu. Malengo ambayo yanatimilika, malengo ya kiuhalisia na malengo yenye muda maalumu." Aliendelea na kusema, "ndoto bila malengo itaendelea kuwa ndoto na kutimilizwa kwake kutaendelea kuwa ni ndoto tu." Mwisho Ndg. Libe aliwaomba wanafunzi hao wasimuangushe kwa kuweka malengo kwenye ndoto zao na kuhakikisha wanazitimiliza.
Liberatusi Mwang'ombe akihutubia wanafunzi shule ya secondary Montfort iliyopo Rujewa, Mbarali
Mbali ya maongezi Ndg. Liberatus alichangia miundombinu ya elimu kwa wanafunzi hao
Moja ya wanafunzi akimshukuru Liberatus kwa kukumbuka alipotoka
Juu na chini Libe akiendelea kubadirishana mawazo na wanafunzi
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

1 comment:

Anonymous said...

poa sana wewe ndo jembe msomi wa kweli one day upinzani wakichukua nchi utapata fursa ya kuwa waziri we elimu au wa uchumi