ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 13, 2015

Afrika yajifungulia mtandao wake wa Afrileaks


Afrileaks utakuwa kamna mtandao wa Wikileaks ambao kazi yake ni kufichua ufisadi



Mtandao mpya mfano ule wa Wiki Leaks , unaolenga kutangaza visa vya ufisadi umezinduliwa barani Afrika. Mtandao huo kwa jina 'Afri Leaks' unanuiwa kutumiwa kulinganisha na kutangaza wazi visa vya ufisadi katika bara nzima.
Kile Afrileaks inaahidi ni mfumo wa hali yajuu wa kama posta mtandaoni ambapo mtu anaweza kuutumia kufichua habari za siri lakini muhimu kwa jamii bila wao wenyewe kujulikana.

Mwenye habari nyeti ataweza kuzipeleka kwa vyombo vya habari kote barani Afrika ambavyo wamejiridhisha navyo kwamba viko huru na wana uhariri wa hali ya juu unaotambulika kimataifa.

Mojawapo ya Maswala yanayowakera wengi ambayo huenda yakapata kuchipuliwa kwa wingi iwapo mfumo huo wa Afrileaks utafana , ni kashfa za ufisadi.
Licha ya kuwa na viwango vya kuridhisha vya ukuaji wa uchumi,Mataifa mengi ya Afrika hata yale yaliyo na utulivu wa kisiasa hupoteza mabillioni ya fedha kila mwaka kutokana na ufisadi uiokithiri, huku taasisi hafifu zikibuniwa bila kuwa na nia ya dhati ya kukabiliana na rushwa. .Ufisadi ni jinamizi kubwa barani Afrika

Lakini Je Afrileaks wataweza kupata umaarufu kama ule wa wikileaks?

Shirika hilo la Afrileaks linasisitiza kuwa halitachapisha habari zozote za kibanfsi za mfichua siri.

Na kwamba lengo lao ni kuwaunganisha wenye taarifa muhimu na waandishi habari wanaoandika makala zilizopelelezwa na kuchunguzwa kwa kina. Pia wameahidi kutoa mafunzo zaidi kwa waandishi habari waliobobea ili kufahamu vyema vipi kuzishughulikia taarifa kama hizo.

Mashirika kadhaa ya habari barani Afrika tayari yameshajisajili na Afrileaks -ikiwemo kutoka nchini Zimbabwe, Mozambique, Angola na Botswana.

Hivyo wenye habari nyeti ambazo alikuwa anatafuta kwa kuzipeleka bila kutambuliwa anahimizwa kuziwasilisha kwa tovuti hiyo ya Afrileaks lakini wanapaswa kufuata utaratibu uliowekwa na wala wasitumie computer za ofisini mwao ili kutotambulika na kujiweka katika hatari.

Je nani atakuwa wa kwanza kujitosa na habari moto moto katika Afrileaks!

No comments: