Kipa mkongwe Ivo Mapunda ameibeba Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kupangua mkwaju wa penalti wa mkongwe Vicent Barnabas.
Mapunda aliingia uwanjani katika dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Peter Manyika ikiwa ni sehemu ya kupewa jukumu la kupangua mikwaju hiyo.
Simba imefanikiwa kushinda kwa mikwaju 4-3 baada ya wachezaji wawili wa Mtibwa kukosa na mmoja Simba Shabani Kisiga kukosa pia.
Kwa ushindi huo, Simba imekabidhiwa kitita cha Sh milioni 10 wakati washindi wa pili Mtibwa Sugar wameondoka na Sh milioni 5.
Simba imekutana na Mtibwa Sugar mara ya pili katika michuano hiyo msimu huu na katika mechi ya kwanza ilifungwa kwa bao 1-0.
Rais wa Zanzibar, Mohammed Ali Shein ndiye alifanya kazi ya kuikabidhi Simba Kombe la Mapinduzi.
CREDIT:SALEHJEMBE
No comments:
Post a Comment