ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 29, 2015

AIRTEL TRACE MUSIC AWARD YATANGAZA TANO BORA

Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kushoto) akitoa ufafanuzi na kulia ni Meneja Masoko Bi Aneth Muga.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando na (wa kwanza kulia) ni Meneja Masoko wa Airtel, Bi. Aneth Muga katikati ni washindi walioingia hatua ya nusu fainali ya shindano hilo.
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa umakini (kushoto).

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel leo imetangaza washiriki walioingia tano bora ya shindano la kusaka na kuibua vipaji vya wanamuziki chipukizi la Airtel Trace Music Star.

Shindano hilo lililozinduliwa rasmi Oktoba mwaka jana, sasa limefikia hatua ya fainali ambapo mshindi wa Airtel Trace Tanzania atapatikana katika fainali inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa Februali mwaka huu.

Mshindi atapata fursa ya kwenda kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Award Afrika, yatakayoshirikisha washiriki wengine kutoka nchi 13 barani Afrika.

(HABARI/PICHA: DEOGRATIUS MONGELA NA DENIS MTIMA/GPL)

No comments: