Moses Iyobo akiwa na mpenziwe ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Na Imelda Mtema/Amani
Dansa mahiri wa staa wa muziki Bongo na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye Moses Iyobo, amefunguka kuwa hakuna kitu kinachompa faraja kubwa kama mimba ya mpenzi wake ambaye ni staa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Iyobo ambaye nyuma kidogo alipost picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kutoa pongezi kwa mpenzi wake huyo kwa kumbebea ujauzito, alisema kuwa hakuna kitu ambacho anaona fahari kama hicho.
“ Mimi tu nikiwaza mtu ambaye ninampenda kwa dhati ana mimba yangu napata faraja kubwa sana hivyo kila siku namuomba Mungu ajifungue salama na ampitishe katika majaribu mazito,” alisema Iyobo.
4 comments:
si aliolwa huyu aunty nasikia au?na mara alikuwa anarukwa na mheshimiwa Fulani mpaka akaenda marekani naya.sasa anaye iyobo,mmmh kazi kweli ipo sasa ile ndoa yake ikoje?
kazi kweli madada wa bongo flava movie
MH!HAYA BWANA IYOBU!KASAFARI KA YU SI AI KAZURI
Usiringe sana, kumbuka huyo ni mke wa mtu. Subiri kufunguliwa kesi ya fidia na kudaiwa mamilioni ya hela kwa uzinzi huo mwenyewe atakapotoka jela.
kumbe aunty umeshindwa kustahamili jamani mumeo yuko jela wewe umeuza mechi mmmma aunty weeeee mmmh vibaya hivyo mtoto wa kike but sikulaumu sana labda alikuwa anakutesaga ndo maana ukaamegeage brother man iyobo
Post a Comment