ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 13, 2015

CHUO CHA MUZIKI CHA TRIPLE J SOUND & MUSIC COLLEGE KIMEFANYA MAHAFALI YAKE YA KWANZA.

Mgeni rasmi Mchungaji Sunday Matondo akitoa hotuba katika mahafali ya kwanza ya chuo cha Muziki cha Triple J. 
Mkurugenzi wa Chuo cha muziki cha Triple j sound & music college, Dk. Leonard Maboko, akizungumza katika mahafali hayo.
Mhitimu wa Chuo cha Triple J akisoma risala kwa mgeni rasmi katika mahafali yao.
Afisa Fedha na Utawala wa Chuo cha Trple J, Mrs Leah Chifunda akitoa utambulisho kwa wageni na wazazi katika mahafali.
Mkuu wa Chuo cha Triple J, Caleb Mwanjoka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya uongozi wa Chuo.
Mgeni rasmi akikabidhi vyeti kwa wahitimu.
Mkurugenzi wa Chuo Dk. Maboko akimkabidhi mgeni rasmi sadaka(limbuko). 
Mkurugenzi akimuonesha mgeni rasmi baadhi ya vifaa katika darasa la vyombo vya muziki.
Wageni waalikwa na wazazi wa Wahitimu wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chuo.
Mmoja wa wanafunzi wanaosoma Chuoni hapo, Nigel Sasali akionesha ufundi wake kwa kuchalaza drums.
Baadhi ya wahitimu wakionesha ufundi wao wa kupiga piano(keyboad) na kuimba mbele ya wazazi na wageni waalikwa.
Mwalimu wa Muziki, Gerald Sizimwa akitoa maelezo kwa Mgeni rasmi na wageni waalikwa. 
Mwalimu wa Elektroniki, Patrik Mwankemwa akiwa kwenye darasa la ufundi akitoa maelekezo kwa wageni.
Mhitimu wa utayarishaji wa mziki, Ambrose Chiwinga, akiwaonesha wageni namna ya kutayarisha na kutengeneza mziki na kurekodi katika Studio ya Triple J baada ya kumaliza mafunzo yake.
Mchungaji Chiwinga akitoa maombi ya kuombea Chuo na uongozi wote ili kupata mafanikio zaidi.
Baadhi ya wageni waalikwa na wazazi wakifuatilia sherehe za mahafali ya kwanza ya Chuo cha Muziki cha Triple J.
CHUO cha muziki cha Triple J Sound & Music college kilichopo Ivumwe jijini Mbeya kimefanya mahafali yake ya kwanza tangu kuanzishwa kwake katika sherehe zilizofanyika chuoni hapo.
Aidha katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi wanne wamehitimu na kukabidhiwa vyeti katika fani za uinjinia wa sauti na utengenezaji wa muziki na watatu katika fani ya upigaji wa vyombo(piano).
Mkurugenzi wa Chuo cha muziki cha Triple j sound & music college, Dk. Leonard Maboko, akizungumza katika mahafali hayo alisema watu wanajishughulisha na sanaa ya muziki ni vema kufanya kazi hiyo baada ya kupata taaluma kutoka vyuoni ili kuboresha tasnia sambamba na kupambana na ushindani wa soko.
Dk. Maboko alisema wasanii wengi wa muziki wanashindwa kuendana na ushindani wa soko kutokana na kukosa elimu ambayo itamsaidia kujua kutumia vifaa, kuandika na kuimba jambo linalosababisha kukosa nyimbo zenye ujumbe kwa jamii.
Alisema kwaya nyingi na vikundi vingi vya uimbaji havina wapigaji wazuri wenye vipaji na taaluma ya muziki pamoja na ujuzi wa uimbaji jambo linalochangia muziki kutokuwa na ubora unaoweza kuleta ushindani na ladha kwa wasikilizaji(hadhira).
Alizitaja kozi zinazotolewa chuoni hapo kuwa ni mafunzo ya kupiga vyombo vya muziki, uinjinia wa sauti na utengenezaji wa muziki, kuimba na kuandika muziki, kozi maalumu ya Software ya muziki iitwayo Pro- tools, utengenezaji wa video, mafunzo ya msingi kwa elektronikia na mafunzo ya awali ya Kompyuta.
Aliongeza kuwa lengo la Chuo hicho ni kuzalisha wanafunzi wenye vipaji na ubunifu watakaoweza kuhimili ushindani na kuinua tasnia ya muziki wa Tanzania hata kufikia ngazi ya kimataifa.
Kwa upande wake Wahitimu katika risala yao kwa mgeni rasmi walisema ni vema viongozi wa vikundi vya muziki, wachungaji na wazazi kuwapeleka watoto wao kujifunza masuala mbali mbali ya muziki ili kuwafanya vijana kuwa wataalamu wa muziki waliobobea.
Naye Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mchungaji Sunday Matondo, ambaye pia ni Mchungaji kiongozi wa Rehoboth International Christian centre, mbali na kupongeza jitihada za Mkurugenzi kwa kuanzisha chuo hicho pia alisema kitasaidia kuongeza ajira kwa vijana.
Alisema hivi sasa kunatatizo la watu wengi kushindwa kufunga vifaa vya muziki katika mikutano jambo linalosababisha kuunguza vifaa hivyo kutokana na uwepo wa Chuo tatizo hilo litaondoka na kuwafanya vijana waliojifunza kuwa keki na kuajiriwa.
Mwisho.
Na Mbeya yetu

11 comments:

Unknown said...

Mawasiliano

Anonymous said...

Naomba namba za simu za chuo kwa mawasiliano zaidi

Anonymous said...

Ada tafadhali

Anonymous said...

Napenda kujiunga na chuo hicho lakin Sina namba ya maelezo maalum au kupata picha halisi na bei ya mihula husika.

Anonymous said...

I need to join in music now

Anonymous said...

Naomba namba ya mawasiliano ase Ili kupata information zaidi??

Anonymous said...

Namba ya simu

Anonymous said...

Kipo mbeya semu gani

ZOMBIE BIG said...

aaah saw ukitaka kujifunza kuanzia kinanda adi kuimba nishingapi

Anonymous said...

Utalatibu wa ada umekaejevnatamani kujua Ili nijiunge n chuo

Anonymous said...

Nahitaji kujiunga nachuo nahitaji muongozo