ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, January 13, 2015

CONVENANT BANK NA AAR KUANZISHA AKAUNTI YA BIMA YA AFYA KUSAIDIA WAJASIRIAMALI

Benki ya wanawake ijulikanayo kama Convenant Bank pamoja na Kampuni ya bima ya AAR washirikiana katika kuanzisha akaunti ya bima ya matibabu kwa wajasiriamali walioko nchini 
Mkutano kati ya Convenant Bank, AAR Insurance na wajasiriamali ulifanyika mwishoni mwa wiki ilopita,uliohusika na kuwaelewesha wajasiriamali kuhusu akaunti hiyo na umuhimu wa bima ya afya kwenye maisha yao ya kila siku.
Akiongea na wajasiriamali Mkurugenzi wa Convenant Bank Bibi Sabeth Mwambenja alisema,“Akaunti hii ya Bima ni maalumu kwa watanzania wote wanaoohitaji kupata bima ya matibabu kutoka AAR,akaunti hii inamuwezesha mmiliki kupata bima ya matibabu na familia yake kwa mwaka mzima kwa shilling 1,000 kwa siku ambayo ni sawa na laki 360,000/= kwa mwaka”
“Benki hii iliwafikria zaidi wajasiriamali na kuona AAR ni kampuni kubwa na uhakika ya afya,lakini tuliona tuombe punguzo kubwa ambalo ni sawa na nusu bei ya gharama ya bima ya afya ya kampuni hii,kwa kua tunatarajia kupata kinamama 120,000 kutumia bima hii”. Alimalizia kusema Bibi Mwambenja.

Pia AAR ilipata nafasi ya kuwashukuru benki ya Convenant pamoja na wajasiriamali wote walofika hapo na kuwapa elimu kuhusiana na bima ya Afya.

Akiongea na wajasiriamali Meneja mauzo, Bibi Tabia Massudi alisema,

“Ni furaha kuwa wamoja katika kutoa mchango mkubwa katika kuwasaidia wajasiriamali,ndio maana hatukusita kukubaliana na suala hili,kwasababu tunajua umuhimu wa afya kwa binadamu na kwa wajasiriamali kama nyie, karibuni sana mpate bima iliyo bora”.


1 comment:

AUGUSTINO YOHANA KORONDI said...

Je nihatua ganinifate ili nijiunge na BIMA HIYO