ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 14, 2015

FASTJET YAKUMBWA NA DHORUBA ANGANI, YASHINDWA KUTUA SONGWE YAGEUZA NA KURUDI DAR


Kiasi cha cha abiria 131 wakiwemo wanawake, vikongwe na watoto, waliokuwa wakisafiri na ndege ya Fastjet, kutoka jijini Dar es Salaam kwemda jijini Mbeya, walikumbwa na taharuki, baada ya ndege hiyo kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, jijini humo, na kubaki ikizunguka tuu kwenye anga la jiji hilo kwa dakika kadhaa.

Hali mbaya ya hewa na ukungu mzito, vimeelezwa kuwa ndio chanzo cha ndege hiyo kushindwa kutua na hata rubani alipofanya majaribio mara mbili ya kutua alishindwa na hivyo kushauriwa na waongoza ndege wa uwanja huo kurejea alikotoka.

Mkazi mmoja wa Mbeya alikaririwa na radio moja ya jijini Dar es Salaam akisema kuwa kwa takriban siku tatu kuanzai Jumapili iliyopita, jiji hilo lililoko nyanda za juu kusini mwa Tanzania, limekumbwa na mvua kubwa inayonyesha mfululizo na kusababisha ukungo mzito angani.
Hata hivyo taarifa zinasema, abiria wote wako salama
Akizungumzia tukio hilo Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe, Valentine Kadera, alikiri ndege hiyo kushindwa kutua kwenye uwanja huo, hivyo kulazimika kugeuza kurudi Jijini Dar es Salaam kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya.

Akizungumzia tatizo hilo, mratibu wa shughuli za Fastjet Mkoa wa Mbeya, Omar Idrisa, alisema ndege hiyo imeshindwa kutua kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hivyo kulazimika kugeuza kurudi Jijini Dar es Salaam mpaka kesho mchana, (Leo Jumanne).

No comments: