Polisi nchini Ujerumani wanasema kuwa kumekuwa na shambuli la kuchoma moto ofisi za gazeti ambalo lilichapisha vibonzo kutoka kwa gazeti la vibonzo la Charlie Hebdo.
Mawe na vitu vinavyowaka moto vilirushwa katika dirisha la ofisi za gazeti la Hambuger Morgenpost mapema leo Jumapili.
Vyumba viwili kwenye afisi hizo viliharibiwa lakini moto huo ulizimwa kwa haraka na hakuna mtu aliyejeruwa.
Baadhi ya nakala zilizochomeka baada ya gazeti la Humbuger Post kushambuliwa
Wiki iliyopita gazeti hilo lilichapisha picha za vibonzo vya mtume Mohammed kutoka gazeti la ufaransa la Charlie Hebdo.
Makala kwenye tovuti ya gazeti hilo inasema haijabainika iwapo shambulizi hilo lina uhusiano na kuchapishwa kwa picha hizo.
Polisi mjni Hamburg wanasema kuwa wamewakamata vijana kufuatia kisa hicho.

6 comments:
watu wanaandamana kulaani consequences na hawaandamani kulaani source. kuna faida gani kuitusi dini ya mtu mwengine? na akikasirika na kufanya tendo baya utasema ugaidi. nadhani dunia imefika wakati tutambue ukijiheshimu nawe utaheshimiwa lakini ukimvunjia heshima mwengine nae atakuvunjia. kuna watu wanahisi wanayo haki ya kutukana wengine kwa kisingizio eti wanafanya mzaha tu au masihara au vichekesho ili kufurahisha jamii huku wakijua fika kwamba hayo ni matusi na yanaudhi na yanaweza kuhatarisha amani let us stop ridicules on others religion, we need to live in peace! God bless the world!!
Wewe uliyeandika hapo una matatizo, huu ndiyo uhuru wa kusema unachotaka. Kuchora vibonzo vya mtu yeyote yule hakuadhibiwi kwa kuuawa......huwezi kuua mtu eti kwa sababu amechora vibonzo......kwani mtu akisema ukristo au uislaam ni mbaya anapaswa kuuawa? Tuwe wastaarabu hizi imani kali za mapokeo hazina maana badala yake watu wamekufa na hao waliohusika wameuawa......eti wanajiita martys?
Wewe anonymous wa kwanza hazipo kichwani na uache ushabiki wa dini,Kwa hiyo hao magaidi kuwaua hao jamaa unaona ama ndio dini yako inakufundisha hivyo, kuwa na roho ya ubinadamu,mungu peke yake ndo anaweza kutuhukumu sisi waja wake according to my religion i don't know about yours.
Wewe anonymous wa kwanza hazipo kichwani na uache ushabiki wa dini,Kwa hiyo hao magaidi kuwaua hao jamaa unaona saw ama ndio dini yako inakufundisha hivyo, kuwa na roho ya ubinadamu,mungu peke yake ndo anaweza kutuhukumu sisi waja wake according to my religion i don't know about yours.
Hapo utaona tatizo liko wapi jamaa hapo juu katimiza hicho mnachodai mkitetea freedom of speech sasa angalia mlivyoanza kumshambulia freedom of speech itakiwi kuvuruka haki za wengine ndio maana ukesema lolote kuhusu holocaust unakwenda jella huwezi kumchora mama yangu u chi ukandiambia freedom intakutandika hachini kushabikia ujinga lol
sadakta anonymous wa 7:14 tuache kushabikia ujinga haya mambo mengine yanalenga kutuletea fujo tu hapa duniani. mbona ukikejeli holocaust utalaaniwa na dunia nzima na hao wanotetea uhuru wa kusema? na sijawahi kuwaona hata siku moja hapa duniani hawa wachora vikatuni wakifanya hivyo basi iwe ni kwa dini fulani au rangi fulani au asili ya watu fulani tu kila siku? mmesahau yule malkia wa urembo wa USA alilazimishwa kujiuzulu taji lake sababu tu katoa maoni yake haamini ndoa za mashoga na anaamini ndoa ya mwanamke na mwanamume?
Post a Comment