ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 16, 2015

Je Wafahamu sifa moja kuu ya Mji wa Dubai?Isome hapa.

Hakuna kitu kizuri hapa duniani kama kuwa na uaminifu kwa mtu, na ikitokea Mtu akakuamini basi unatakiwa kufanya juu chini asipoteze uaminifu wake kwako kwa maana uaminifu wake ukipotea basi ni kazi kubwa sana kuurudisha. Uaminifu huo ndio ulioifanya Dubai kuwa Moja Mji hapa Duniani kuaminika.
Hii imetokea Huko Dubai ambapo Sifa moja hii ya Imani imepelekea Dubai kujinyakulia sifa moja tu katika Miji yote Hapa Duniani.
Mara baada ya Mtengenezaji wa Filamu kutokea Uingereza katika mitaa ya Dubai kuendesha utafiti wake alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake.
Mtengeneza filamu huyu ajulikanae kwa jina la Daniel Jarvis, mwenye umri wa miaka 26 alificha kamera yake na kuweza kurekodi mfululizo wa matukio ya makusudi ya kuokota pochi hiyo na wasamaria wema hao kurudisha pochi hiyo kwa muhusika huku akiwa pamoja na rafikiye aliyejipachika jina la utani la 'Digi' ama Dan, mwenye miaka 25, walibarizi katika viunga vya Downtown na Bur vilivyoko Dubai,siku za karibuni.Mara baada ya mfululio huo wa kurudishiwa pochi yake Mtengeneza filamu huyo aliuliza swali "Je unaweza Kuiba Dubai?" yote hiyo ni katika kuendelea kuichunguza jamii. Aliweza kurusha vipande vyake vya video katika mtandao maarufu wa Youtube ambapo mpaka kufikia Jana usiku Watu takribani 70000 waliweza kuangalia vipande hivyo.
Mtandao wa 7 DAYS ulishangazwa sana na utafiti huo huku kitu kikubwa kilichowashangaza ni waokotaji wa pochi hiyo waliweza kuokota bila kujishughulisha kutazama ndani kuna nini?ilhali pochi hiyo ilikuwa imejaa Euro na pesa ya falme za kiarabu ya Dirham
Utafiti wa kwanza ulifanyika katika mtaa wa matajiri uliopo katika barabara ya Sheikh Zayed karibu na soko kuu la kibiashara na jirani kabisa na mnara wa Emirates lakini kila aliyeiokota pochi hiyo aliirejesha kwa mwenyewe huku baada mtengenezaji huyo akifikiri kuwa sababu ikiwa ni mtaa wa matajiri.
Utafiti ukahamishiwa Mtaa wa pili katika eneo lijulikanalo Bur ,Dubai, mtaa ambao ulionekana ni mtaa wa watu wa kipato cha chini lakini cha ajabu watu waliendeleza utamaduni ule ule wa kurejesha pochi kama ilivyo, na hali eliendelea hivyo mara kadhaa.
Utafiti huo haukuwa wa kwanza kufanywa na Jarvis, Jarvis anasema utafiti kama huo alishawahi kuufanya katika mji wa London nchini Uingereza. Na huko walistaajabu walipoidondosha tu aliyeiokota alianza kukimbia nayo.
Mara baada ya kumaliza utafiti huo katika nchi za Falme za Kiarabu, Utaendelea kufanywa pia katika nchi za Amerika, Ulaya na hatimaye Afrika kuona ni nchi gani itaweza kuvunja rekodi ya Dubai.
Swali unahisi ni Nchi gani ambayo itavunja rekodi ya Dubai?.
 Credit:LUKASA

2 comments:

Anonymous said...

waje wakafanye pale mjengoni kwa mkulu na bungeni na wapite manzense na uwanja wa visi waishiye bukoka.

watueleza matokiyo walikuwaje. haaaaaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

wazungu wezi kama tulivyo sisi miafrica na waarabu si wezi ndo maana pochi yake alikuwa anarudishiwa bila kuchomolewa au kuchukuliwa chochote kila.

na mlio na chuku na waarabu mnajisumbua bure.kaeni na wezi wenzenu wazungu