ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 16, 2015

Kisomo cha kumuombea Rashid Mkakile apone haraka ni January 17, 2015(Boston, MA)

A.Alaykum, nategemea mnaendelea vizuri katika shughuli zenu za kila siku kwa uwezo wake Allah
Nilikuwa nawajuulisheni kuwa kutakuwa na kisomo cha kumsomea Ndugu yetu Rashid Mkakile ambaye ni mgonjwa alikuwa amelazwa Hospital ya Beth Israel Deaconess Medical Center na sasa hivi yupo kwenye Physical therapy kwa ajili ya Recovery, lakini bado ni mgonjwa
Tunamuomba Mungu ampe uzima wake na duwa zenu zinahitajika

Tunawaomba kwa kila mwenye uwezo wa kuja kusoma kwa pamoja itakuwa vizuri na kisomo kitafanyika siku ya Jumamosi 1/17/2015 Kuanzia 4:00PM to 7:00PM

Address ya ukumbi ni
10 Putnam St,
RoxburyMA 02119

Zaidi unaweza kuwasiliana na
Ikota. 240-988-0359

Nyote mnakaribishwa.

6 comments:

Anonymous said...

jamani ndugu zangu waislam wenzangu napenda turekebishane wala si ugomvi naomba mnielewe kwanza kabisa pole mgonjwa na nazidi kukuombea kwa allah afya yako izidi kuimarika ishala ,sasa nakuja kwenye hiki kitu kisomo sifikiri ni kitu kizuri mnavyo weka kwenye mitandao kwamba kuna kisomo cha kukuomba nafikiri ingekua vizuri kwa aina ya kisomo hiki mkajichukua wana familia wenyewe na watu wa wili watatu na mashehe mkafanya nyumbani inatosha .kwasababu kunawatu wengine imefikia kipindi hadi wanafikiria huyu mtu anafanyiwa kisomo cha hadhara na mnahii kwani amefariki kwahiyo naombeni msichukuli hii kitu person ni kurekebishana tuu .

Anonymous said...

hata mie nimestuka nilidhani ame-rest...

Anonymous said...

Wanamchukia vibaya sana mdogo wetu Rashidi mimi mwenyewe nilivyoona tangazo vijimambo kuhusu kisomo cha bwana Rashid kabla hata sijaanza kusoma chochote chini nikaanza kupiga kelele na kuingia straight kwenye internent kukata ticket ili niende kwenye msiba wa Rashidi nikaanza kulia sana cause nimeishi naye vizuri sana hapa DC ni rafiki yangu wa toka nikutoke ndiyo mume wangu kusoma Habari yote na kuniambia no hajafariki ni Habari kuhusu kisomo tuu.Jamani ndugu zangu na wadogo zangu wapendwa Ikotta na Isca please huyu kaka anahitaji maombi ya kifamilia na muacheni Allah aitwe Allah na afanye kazi yake. Rashidi kaka yangu utapona kwa jina la Allah.Mungu azidi kukuona hapo ulipolala na akupe nguvu zote Utanyanyuka kwenye hicho kitandani ulicholala.Amen

Anonymous said...

Nimeimanisha hapo juu kuwa wanamchulia vibaya na nimkosi mkubwa sana.Muogopeni Mungu jamani

Anonymous said...

Good point mdau hapo juu, Feel better brother Rashid Mkakile Mungu atakusaidia Insha allah!

Anonymous said...

Ikotta na Isca toweni hilo tangazo kwenye vijimambo wadau wote hapo juu na comments zao wametoa points nzuri sana mpaka huyo mdau wa nne ameandika kwa hisia sana na kuanza kulia knowing Mtu wake wa karibu sana Rashidi Mkakile ameshatangulia kwenye haki za Mungu, nyie wana ndugu wenzangu Ikotta na Isca hamuoni hiyo tayari ni mkosi mkubwa? Toweni hilo tangazo tafadhali muombeni nyie wenyewe kama familiya na mimi mwenyewe binafsi namuombea rafiki yangu Rashidi kila siku ya Mungu apone na apewe nguvu za Mwenyezi Mungu.Remember maneno ya wengi hutokea kiukweli mtamzika kabla ya siku zake kufika. Ni hayo tuu Again TOWENI, TOWENI NASEMA TENA TOWENI JAMANI HILO TANGAZO NI LA MSIBA NA RASHIDI BADO YUKO HAI, MNAMCHULIA KAKA WA WATU NI DHAMBI KUBWA MNOOOOO.