Hayyat Mfalme Abdullah
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa mfalme wa Saudi Abdullah bin Abdulaziz amefariki dunia akiwa hospitalini .
Tamko la kifo cha mfalme huyo zilitolewa na kaka wa mfalme huyo aitwaye , Salman,ambaye naye aliwahi kuwa mfalme.
Kabla ya tamko hilo television ya taifa la Saudi lilikatiza matangazo yake na kuweka nyimbo za quraan ,kama ishara ya kifo cha kiongozi wa juu wa ufalme.
King Abdullah, amefariki dunia akiwa na miaka 90, alilazwa hospitalini kwa wiki kadhaa tangu December mwaka wa jana kutokana na maambukizi kwenye njia ya hewa.
Mfalme huyo aliingia madarakani mwaka 2005 lakini alikuwa ni dhaifu mwenye kushambuliwa na maradhi mara kwa mara.-BBC
3 comments:
Qur an haina nyimbo ndugu muandishi,unapotaka kuandika jambo tafuta elim yake kwanza na sio kutuandikia tu...QUR AN na nyimbo ama what we call QASIDA ni tofauty....Maneno matukufu ya ALLAH utayaitaje nyimbo?
kwani tatizo ni nini? kikubwa ujumbe umewafikia watu.well kwa sisi watu wa dini nyingine tusemeje sasa? don't complicate.
inna lillahi waina illahim rajiun.
Post a Comment