ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 22, 2015

MUASISI WA TANU AAGWA MONDULI

Waziri mkuu wa zamani mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa na mkewe mama Regina Lowassa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.Mzee Ole Ngoilenya ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 120 alikuwa muasisi na kiongozi wa kwanza wa Chama Cha TAA na baadaye TANU wilayani Monduli wakati huo ikijulikana kama Maasai District.Pia ndiye alikuwa chachu kwa Mh Lowassa na wanasiasa wengine wa Monduli kuingia katika siasa. Alioa wake 9 na kufanikiwa kupata watoto 53.
Waziri mkuu wa zamani mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa na mkewe mama Regina Lowassa wakitoa pole kwa wafiwa baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mzee Lazaro ole Ngoilenya Laizer aliyefariki juzi na kuzikwa leo Alhamis kijijini kwake Ngarash Monduli.

No comments: