Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa, Tumaini Msowoya akimkabidhi msaada mmoja kati ya wagonjwa waliolazwa katika Wodi ya watoto kwenye Hospitali ya mkoa, wakati alipotembelea wodi ya watoto 22.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Iringa, Tumainia Msowoya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoani Katavi, William Mbongo na Katibu wa UVCCM Wilayani Mufindi, Kantala, wakiteta jambo.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Wakati watanzania tunaanzimisha miaka 51 ya mapinduzi ya zanzibar, mwenyekiti wa vijana ccm mkoani Iringa TUMAINI MSOWOYA ambaye ni mke wa mgombea ubunge jimbo la iringa mjini na ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Frank Kibiki amewataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MSOWOYA amesema kuwa wanawake wawemstari wa mbele kuchukua fomu za kugombea na kwamba wasikatishwe tamaa na baadhi ya watu wanaodhani kwamba wanawake hawawezi kugombea na kuongoza katika nafasi mbalimbali.
Aidha ameongeza kuwa Jamii iachane na mitazamo tofauti kwa wanawake wanao jitokeza kugombea nafasi za uongozi na kuwaasa wanawake wawe na misimamo pindi wanapoingia madarakani, kujiamini na kutokubali
kutumiwa kama chombo cha starehe.
Mbali na hayo MSOWOYA amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
Ameendelea kusema kuwa vijana wajotokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.
Amemaliza kwa kuwapongeza vijana wa ccm mkoa wa Iringa kwa kuazimisha siku ya mapinduzi ya zanzibar kwa kufanya shughuri za kijamii ikiwamo kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya manispaa.
No comments:
Post a Comment