Wafanyakazi wa BBC wakiwa kazini,Tulanana Bohela wa Focus on Africa na Halima Nyanza wa BBC Swahili wakimhoji waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe.
Serikali ya Tanzania imeunda kikosi maalumu kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ukatili wanaofanyiwa watu wenye ulemavu wa ngozi –Albino- na huku ikitangaza pia kupiga marufuku kuanzia leo wapiga ramli wote ambao wanaelezwa kuchangia mauaji ya watu hao.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe Ameitaja mikoa inayotarajiwa kuanza kwa operesheni maalum ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya walemavu katika juhudi za kukomesha kabisa matukio hayo, ambayo yameelezwa kuanza kuibuka tena.
Mikoa hiyo ni Mwanza, Simiyu, Geita, Tabora na Shinyanga.Operesheni hiyo pia inatarajiwa kuendelea katika mikoa mingine.Aidha amesema operesheni hiyo itaanza baada ya wiki mbili kwa ushirikiano wa polisi na wawakilishi kutopka chama cha watu wenye ulemavu Tanzania.
Kazi ya kikosi hicho ni pamoja na kupitia pia kesi zote zilizowahi kufikishwa mahakamani kuhusiana na vitendo hivyo.kizungumzia kuhusiana na kupigwa marufuku kwa wapiga ramli nchi nzima, Waziri Chikawe amesema jeshi la polisi litaandaa operesheni maalum kuwatafuta na kuwashtaki.
Amesema wapiga ramli hao wanajulikana na wananchi wanaomba kusaidia kuwatambua.
Aidha amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo zima, ikiwemo pia kuyataka madhehebu ya dini mbalimbali na mashirika ya kijamii kutoa elimu juu ya jambo hilo.Sababu kubwa iliyotajwa inayosababisha watu kutafuta viungo hivyo vya binadamu inaelezwa kuwa ni kupata utajiri.
No comments:
Post a Comment