ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 22, 2015

MWIGULU NCHEMBA AZINDUA HUDUMA MPYA BENKI YA MAENDELEO YA KKKT

Naibu waziri wa fedha, Mwigulu Lameck Nhemba, (Kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Kanisa la Kiluteri la Kiinjili Tanzania, (KKKT), Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, wakati alipozindua huduma mpya ya benki hiyo ijulikanayo kama "MB Mobile". Huduma hiyo itamuwezesha mteja wa benki hiyo inayomilikiwa na KKKT, kuweza kufanya miamala mbalimbali kupitia simu ya mkononi. Miamala hiyo ni kama vile, kuweka fedha, kujua salio kwenye akaunti, kuhamisha fedha toka kwenye akaunti yako, kununua luku, kuangalia taarifa fupi ya akaunti yako na kupata taarifa ya miamala yako. Uzinduzi huo ulifanyika leo Alhamisi Januari 22, 2015
Naibu waziri Nechemba, na mkurugenzi mtendaji wa benki ya Maendeleo, Ibrahim Amulike Mwangalaba(Kulia), wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa huduma hiyo, huku Mkuu wa KKKT, Dkt. Malasusa, akishuhudia
Dk. Malasusa, (Katikati), naibu waziri Nchemba, (Kulia) na katibu wa bodi ya benki hiyo, Balozi Richard Mariki
Dkt. Malasusa akitoa hutuba yake
Mkurugenzi Mwangalaba akitoa hotuba yake
Naibu waziri Nchemba, akitoa hotuba yake
Viongozi wa KKKT
Wageni na viongozi wa benki hiyo
Naibu waziri Mwigulu Nchemba, akionyesha zawadi ya tuzo aliyopewa na benki hiyo ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwenye sekta ya fedha
Akikabidhiwa zawadi hiyo
Picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya benki hiyo
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog

No comments: