MZIMU wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, limeendelea kuwatafuna watuhumiwa wa uchotwaji wa mabilioni ya fedha za akaunti hiyo baada ya watuhumiwa wengine watatu kupandishwa mchana huu kizimbani katika mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Waliopandishwa ni Meneja wa Misamaha ya Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Leonard Mutabingwa ambaye anadaiwa kupokea rushwa ya zaidi ya shilingi bilioni moja kama zawadi kutoka kwa Rugemalira, Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Mkombozi , Julius Ruta, ambaye anadaiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 100 pamoja na Ofisa Mwandamizi wa Tanesco, Steven Urasa, anayetuhumiwa kupokea zaidi ya shilingi milioni 100.
Mpaka GPL inatoka mahakamani hapo ni mtuhumiwa mmoja tu aliyefanikiwa kuwa nje kwa dhamana ya kuweka nusu ya fedha anazotuhumiwa kupokea akitakiwa kuwa na watu wawili kama wadhamini. Watuhumiwa wengine walishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi zao kutajwa tena tarehe 27, 29 Januari na 11 Februari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment