Kitendo cha kiungo Shabani Kisiga kimesababisha kifo cha shabiki mmoja wa Simba jijini Dar es Salaam.
Kisiga alikosa penalti wakati wa fainali ya Kombe la Mapinduzi jana dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo iliisha kwa Simba kushinda kwa mikwaju 4-3.
Kukosa kwa Kisiga kulifanya Simba iwe katika hatihati ya Simba kulikosa kombe hilo na inaelezwa mtu huyo alianguka na kuzimia na baadaye alipoteza maisha.
Awali ilielezwa ni eneo la Mburahati, wengine wakaeleza ni Tegeta.
Mtu mmoja alihojiwa na redio ya E FM na kusema aliyefariki dunia ni baba yake mdogo.
“Hakuwa na tatizo lolote la afya, hata wakati anakwenda kuangalia mpira kwenye runinga alikuwa safi.
“Baadaye tukaletewa taarifa kwamba alianguka baada ya Kisiga kukosa penalti,” alisema.
Taarifa zinaeleza mwili wa marehemu utasafirishwa kesho kwenda kwao Mbeya.
CREDIT:SALEH JEMBE
No comments:
Post a Comment