ANGALIA LIVE NEWS

Friday, January 30, 2015

Tanga kuwa na timu tatu Ligi Kuu ijayo?

Kikosi cha Costal Union ya Tanga 

Timu za Tanga zilizopo Ligi Kuu kwa sasa ni Coastal Union na Mgambo JKT.
IWAPO African Sports itafanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara, basi Mkoa wa Tanga utakuwa na timu tatu kwenye ligi hiyo msimu ujao.
Timu za Tanga zilizopo Ligi Kuu kwa sasa ni Coastal Union na Mgambo JKT.
African Sport inaongoza Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza ikiwa imecheza michezo 19 huku ikibakiza mitatu kufunga hesabu.
Kanuni za Ligi hiyo zinasema kuwa timu mbili zitakazomaliza ligi hiyo kwenye nafasi za juu kwenye kila kundi, zitapanda Ligi Kuu na hali ilivyo African Sports wamejiweka pazuri kwani wanahitaji pointi nne pekee.
Kama timu hiyo itashinda mchezo mmoja na kutoa sare mmoja tu itafikisha pointi 45 na tayari itakuwa imefuzu kushiriki Ligi Kuu kwani hakutakuwa na timu nyingine ambayo itaweza kupita pointi hizo.
Katika hatua nyingine, mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu 2014/15 unakaribia tamati na mpaka sasa Coastal Union ipo kwenye nafasi ya tano ikiwa kwenye pointi 16 wakati Mgambo wako kwenye nafasi ya tisa ikiwa na pointi 14.
Hali hii inaashiria kuwa iwapo timu hizo zitaendelea kubaki basi uhasimu wa Coastal na African Sports kwenye soka utafufuka.
Source:Mwanaspoti

No comments: