Katika hadithi ifuatayo
iliyosimuliwa na Abu
Dawood na Ibni Majah
hadithi ambayo Sheikh Al
Albani ameitaja kuwa ni
"hadithi njema", na hadithi
hii pia ni dalili kwamba
elimu ya kutabiri kwa nyota
ambayo huandikwa katika
magazeti na watu hupenda
kusoma kwa kutaka kujua
bahati zao, kitendo hiki ni
atakayesoma nyota yake,
basi swala zake hazikubaliwi
kwa muda wa siku arobaini,
hii ikiwa anasoma na huku
haziamini, amma akisoma
na huku anaziamini, basi
anaingia katika hukumu ya
aliyemuendea mtabiri na
kumuuliza jambo, na
anakuwa amekwisha kufuru
yote aliyoteremshiwa
Muhammad (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam).
Mtume (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam)
amesema:
"Atakayejifunza sehemu ya
elimu ya nyota (utabiri)
amejifunza sehemu ya
uchawi, akiongeza
atakachoongeza (katika
uchawi au nyota)."
Na hii ni kwa sababu
wanaosoma elimu ya nyota
(utabiri) wanaamini kwamba
katika nyota wanaishi majini
ambao ni masultani na
wakuu, na wanaitakidi kuwa
mambo yetu yote
husababishwa na harakati
za nyota hizo kila
zinapotaharaki kutoka
mahali kuelekea pengine.
Kwa ajili hiyo wao huzingoja
nyota hizo masaa mengi ya
usiku ili wapate kuandika
talasimu zao, na huku ni
sawa na kuziabudu nyota
hizo.
(Pana tofauti baina ya elimu
ya anga za juu (Astronomy)
ambayo haina ubaya
wowote ndani yake, na elimu
ya nyota (Astrology) -
utabiri - ambayo ni
haramu).
Ushahidi Mwengine
unapatikana katika hadithi
iliyosimuliwa na Umran bin
Hussain (Radhiya Llaahu
‘anhu) aliyesema kwa
Mtume (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam)
amesema:
“Hayuko pamoja nasi
mwenye kuamini juu ya
nukhsi ( waarabu walikuwa
wanapotaka kusafiri
humrusha ndege na
akielekea upande wa kulia
basi husafiri, amma
akielekea upande wa
kushoto huamini ni ukorofi
na kuivunja safari yake), na
pia hayuko pamoja nasi
mwenye kupiga ramli au
mwenye kupigiwa, na
atakayemuendea mtabiri na
akamsadiki asemayo basi
kesha kufuru yale
aliyoteremshiwa Muhammad
(Swalla Llaahu ‘alayhi wa
sallam)."
Al Bazaar.
Katika hadithi hizi Mtume
(Swalla Llaahu ‘alayhi wa
sallam) anatukataza
tusiwaendee wachawi wala
watabiri wa aina yoyote ile
kwa kuwauliza juu ya jambo
lolote lile, hata kama
atajibadilisha na kujiita
AlHajj Fulani au Sheikh
Fulani au Maalim Fulani au
Mganga Fulani na hii ni
kutokana na kufru zao
wanazozifanya kwa
kuwasujudia majini na
kuridhishana nao ili
wawatumikie.
Na hii ni dalili kwamba
uchawi upo, maana kama
haupo, basi Mtume (Swalla
Llaahu ‘alayhi wa sallam)
asingetukataza kufanya
kisichokuwepo.
Pia hadithi hizi
zinatufahamisha kwamba
mambo haya ni haramu na
atakayeyatenda anakuwa
amekwishayakanusha yale
aliyokuja nayo Mtume
Muhammad (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam) kwa
sababu aliyokuja nayo
Mtume (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam) ni
kwamba hapana aijuwae
ghaibu isipokuwa
MwenyeziMungu
Subhaanahu wa Taala.
Hadithi ziko nyingi sana,
lakini hizi pamoja na aya
zilizotangulia zinatosha
kuwa ni dalili kwamba yote
hayo yametajwa katika Qur-
aan na katika mafundisho ya
Mtume (Swalla Llaahu
‘alayhi wa sallam).
2 comments:
sasa mmekusudia nini kwa kuweka habari hii nimeshaiona imejirudia rudia zaidi ya mara mbili.
choko choko mchokoeni pweza binadamu hamtomuweza
kaka luke napita tu, angalia chokochoko hizo upande wa pili wasije wakakufrench
Post a Comment