Mfanyabiashara, Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa amefungwa kamba na watesi wake.
Stori: Musa Mateja GPL/Risasi
HATIMAYE ukweli wa kutekwa, kuteswa kwa kudhalilishwa kwa aliyekuwa mume wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhan ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’, umejulikana, Risasi Jumamosi limechimba.
Januari 28, mwaka huu, picha za Tevez akiwa ametoka kuteswa kwa kudhalilishwa zilisambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii huku wengine wakidai kisa ni kukutwa na mke wa mtu, wengine wakisema ni dhuluma.
RISASI LAINGIA MTAANI KUCHIMBA
Risasi Jumamosi halikufanya haraka kuichapisha habari hiyo mpaka kuichimba kwanza ili kujua kisa na mkasa kamili ndipo iwapelekee wasomaji wake. Na ndivyo ilivyofanyika!
Risasi Jumamosi lilichimba na kubaini kuwa, tukio la Tevez kufanyiwa ukatili huo lilitokea kwenye mji wa Durban nchini Afrika Kusini ambako alikwenda kibiashara.
“Tukio si la Dar kama wanavyosema wengine, limetokea mjini Durban, Afrika Kusini. Si unajua jamaa (Tevez) ni mtu wa tripu za kibiashara!” alisema mtoa habari mmoja akiomba hifadhi ya jina lake.
Jeraha likiwa mgongoni mwa Jumanne Hassan ‘Tevez’ baada ya kuteswa.
WALIOFANYA UKATILI
Kwa mujibu wa chanzo hicho, watu waliomtenda Tevez ni jamaa zake anaofanya nao biashara ambayo Risasi Jumamosi halijaijua vizuri (ingawa kwenye mitandao ya kijamii wanadai ni madawa ya kulevya).
YATAJWA DHULUMA
Chanzo kikaanza kuanika historia nzima tangu Tevez hajafanyiwa utekaji na udhalilishwaji huo.
“Siku za nyuma Tevez alipewa mzigo nchini Tanzania ili awapelekee hao jamaa wa Afrika Kusini. Aliondoka jijini Dar kwenda Nairobi, Kenya kwa basi akiwa na begi.
“Alipofika Nairobi, ilidaiwa begi hilo alilisahau kwenye basi lakini wengine wanasema aliuuza Nairobi na kwenda Afrika Kusini akiwa na begi feki.”
TEVEZ AWASILI AFRIKA KUSINI, AKUMBANA NA MSALA
Habari zaidi zikachimbuka na kudai kwamba, Tevez aliwasili mjini Durban na kukutana na jamaa zake ambapo aliwaambia mzigo aliusahau kwenye basi.
“Kumbe inasemekana jamaa aliyemuuzia mzigo Nairobi anafahamiana na jamaa wa Sauz na aliwapigia simu kuwaambia kwamba, ameuziwa mzigo na Tevez.
“Kwa hiyo mpaka Tevez anawasili kule, jamaa walikuwa wanajua hana mzigo kwa kuwa aliuuza Nairobi,” kilisema chanzo.
‘Tevez’ akiwa na moja ya wadau wenzake katika biashara anazofanya huko Durban.
ATEKWA, ADHALILISHWA
Ikaendelea kudaiwa kuwa, madai ya Tevez yaliwakera jamaa kwa vile walijua kila kitu, hivyo walimteka na kuanza kumtesa kwa kumvua nguo zote, wakamfunga kamba za manila za rangi ya bluu na kuanza kumtesa kwa adhabu mbalimbali ili kumkomesha.
Inadaiwa katika adhabu hiyo, jamaa hao walimpiga na kitu chenye ncha kali hali iliyosababisha Tevez atokwe na damu na ngozi kuchubuka eneo la mgongoni.
MADAI WAKATI WA UDHALILISHWAJI
Inadaiwa wakati udhalilishaji huo ukiendelea, jamaa hao walikuwa wakisema wanachotaka ni mzigo wao na si kitu kingine.
MARAFIKI, JAMAA WA DAR
Kufuatia kusambaa kwa picha hizo mtandaoni, marafiki na jamaa wa Tevez waliopo Bongo walilazimika kufanya mpango kwa kuwasiliana na watu wa karibu waliopo Durban kumnusuru Tevez kwa kumpeleka hospitali ambako anapata matibabu hadi juzi, Alhamisi.
Risasi Jumamosi: “Kuna habari alikatwa sehemu za siri ni kweli?”
Chanzo: “Si kweli.”
Risasi Jumamosi: “Inasemekana alifanyiwa kitu mbaya cha mambo ya Sodama, ni kweli?”
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’ akiwa na moja ya jamaa zake sauzi.
RISASI LATINGA DUKANI KWA MKEWE WA SASA
Ili kuzidi kupata habari zaidi, Januari 28, mwaka huu, usiku Risasi Jumamosi lilikwenda Kinondoni Kwamanyanya, Dar kwenye duka la mke wa sasa wa Tevez ili kumsikia anasema nini kuhusu tukio hilo.
Paparazi wetu hakumkuta mke huyo lakini alibahatika kuongea na msichana aliyekuwa nje ya duka hilo na kumuuliza aliko Tevez.
Msichana: “Tevez yupo safarini Morogoro.”
Risasi Jumamosi: “Mbona hapatikani hewani? Nipe namba zake nyingine.”
Msichana: “Nilizonazo ndiyo hizohizo ulizonazo wewe, ni…(akazitaja).”
Kweli namba hizo ndiyo alizokuwa nazo paparazi wetu.
MAMA MKWE WA TEVEZ
Kesho yake, Risasi Jumamosi lilimsaka kwa simu mama mkwe wa zamani wa Tevez (mama wa Isha) lengo ni lilelile, kutaka kujua kama naye ana taarifa hizo na anasemaje.
“Ni kweli nimesikia na nimeona picha zake yaani nimesikitika sana kiasi kwamba nikawa siamini kama ni kweli yeye anaweza kufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
“Kikubwa namshukuru Mungu kusikia yupo hai na kwa maana hiyo namuombea zaidi ili arudi katika afya yake,” alisema mama mkwe huyo aitwaye Rukia Juma.
Bw. Jumanne Hassan ‘Tevez’akiwa na mkewe.
MTU WA KARIBU NA TEVEZ
Risasi Jumamosi liliendelea kutafuta undani zaidi wa tukio la Tevez kwa kuongea na watu wake wa karibu waliopo Durban, ndipo likapenyezewa ishu mpya kuwa, baadhi ya ndugu na wafanyabiashara wenzake na Tevez wamechanga na kurudisha mali zilizokuwa zikidaiwa na jamaa hao.
“Nilikuwa Durban muda si mrefu na hapa ndiyo narejea nyumbani (Bongo). Kiukweli tukio la Tevez ndiyo habari ya mjini Sauz, maana jamaa wamemfanyia mbaya kinoma lakini kusema kweli hajakatwa nyeti kama mitandao ya kijamii inavyoandika, wamempiga sana.”
“Kingine ambacho ninajua tayari ameshatolewa kwenye jengo alilokuwa ametekewa na sasa yupo hospitali maalum ambayo siwezi kukutajia, ila huenda hali yake ikawa nzuri kama kweli atakuwa chini ya uangalizi wa madaktari,” alisema jamaa huyo.
Source:GPL
5 comments:
aaah aaah wapi bwana ni kweli amakatwa nyeti yake na pia amafanyiwa kitu mbaya unadhani watu watasema kweli na picha yake hii mmeiziba lakini kuna mitandao kibao inaionyesha na sehemu za nyeti yake inavuja damu acheni acheni kutupiga fix.
tunampa pole lakin jamani dhulumu mbaya sana tena uwazulumu waauza ungaa wenzako utakiona cha mtema kuni.
lakin tunammpa pole na kukatwa nyeti ni balaaaa utamu wote atakosa sasa pole sana mkuu
semeni kweli msifiche jamaa kafanyiwa kitu mbaya sana
mapusher balaa na mwisho wa kuuza sembe mmafanikio yake ndo haya.
nyeti puuuuu mchezo mbaya pwaaaa. balaaaa juu ya balaaa
kudadeki tayari wameshamshughulikia amezulumu pesa na wao wamemfanyia kitu mbaya mbaya sana na nyeti katwaaaa.. dudadekii duuu pole sana kaka
walivyokua wanatesa njia mmoja wapo walimgegeda kwanza haafu ndo wakakata nyeti.
habari hii wanakanusha kwa vile haya ndo yaliyotokea na ni ya aibu sana ndo maana hawasemi ukweli.
mkewe nasikia hana hamu na wa south.chezee kwa baba mandela wewe
mapunda wawafanyi wabongo kwa wabongo wenzao si kwa masouth.
pole sana tevez
ni mmoja kati ya matukio yenye kufedhehesha sana tena sana;maskini sijui uso wake atauweka wapi si bure anaweza akajiuwa. mimi nashauri akipona tu apewe counseling.
Daaaah pole sana kaka yote maisha kutafuta nisawa na vitani ila usijali yote kwa yote ni kushkuru mungu upo hai vingine vyote vinatafutwa tunakuombea mungu upoe kwa haraka bro hilo ndo lakuomba kwa sasa maneno maneno hayatasaidia kitu!
Post a Comment