Polisi wakiwaandama wanaume waliokuwa wamejihami na waliowaua wandishi wa habari wa jarida la Charlie Heblo
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kwamba washukiwa wawili waliohusika na mauaji ya Charlie Hebdo wameuawa.
Wawili hao walisakwa kwa siku mbili na polisi baada ya kutoroka baada ya kuwaua wandishi habari wa jarida la Charlie Heblo.
Maafisa wa usalama walivamia eneo ambako vijana hao walikuwa wamejificha wakiwa na mateka mmoja na kuwaua vijana hao ambao walikuwa ndugu.
Milio ya risasi ilisikika huku moshi mkubwa ukionekana kufuka kutoka katika jengo hilo huku makomando wakionekana wakivamia jengo hilo.
Duru zinasema washukiwa hao walikuwa wamejihami walifyatulia risasi makomando hao kabla ya kuuawa.
Walisema waliwaua wandishi wa habari kama hatia ya kulipiza kisasi hatua ya wahariri wa jarida hilo kuchora vibonzo kumkejeli mtume Mohammed wa dini ya kiisilamu.
Iliarifiwa walikipora kituo cha mafuta wakiwa mbioni huku wakiwateka mateka na kwenda nao katika kiwanda ambako walikuwa wamejificha.
Mateka mmoja aliweza kuokolewa.
Kwingineko milipuko na milio ya risasi ilisikika ndani ya duka la jumla la kiyahudi, Kaskazini mwa mji huku watu watano waliokuwa wametekwa nyara na mshambuliaji mmoja wakiuawa.
Baada ya operesheni ya polisi kukamilika baadhi ya matyeka wlaiokuwa wamezuiliwa ndani ya duka hilo walionekena wakitoka nje.
No comments:
Post a Comment