Waziri Harrison Mwakyembe akila kiapo ndani ya Bunge la Afrika Mashariki, Arusha.
Siku chache zimepita tangu yatangazwe mabadiliko madogo ndani ya Baraza la Mawaziri Tanzania.
Aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amehamishwa na kwa sasa ni Waziri wa Uchukuzi wakati Waziri Harrison Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi kabadili kwenye nafasi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Leo kuna taarifa kwamba Waziri huyo ameapishwa katika Bunge hilo Arusha na kuahidi kushughulikia kero zote zinazoikabili Wizara hiyo kama ambavyo alifanya kwenye Wizara ya Uchukuzi.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel F. Kidega akimpongeza Waziri Harrison Mwakyembe ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Daniel F. KIdega na Waziri Harrison Mwakyembe.
Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Abdallah Sadaala Abdullah (kushoto) akiwa na Waziri wa EAC Uganda, Shem Bageine (aliyekaa katikati) pamoja na Waziri wa EAC Tanzania, Dk.Harrison Mwakyembe (kulia).
Asante kwa Rweyunga Blog kwa hizi picha. Na Millard Ayo.com
No comments:
Post a Comment