ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 15, 2015

ZARI ALALA KWA MAMA DIAMOND

Mrembo wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’.


Stori: Mwandishi Wa/ Amani
IMEFICHUKA! Mrembo wa Uganda ambaye kwa sasa ndiye ‘usingizi’ wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ hivi karibuni alitua Bongo na kulala nyumbani kwa mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’, Sinza-Mori jijini Dar.
Chanzo makini kilicho karibu na familia ya Diamond kimepenyeza ‘ubuyu’ kuwa, Zari alipata fursa ya kupiga ‘mbonji’ nyumbani hapo alipomtembelea Diamond.

“Alikuja akambonji kwa mama Diamond kama siku mbili hivi halafu wakaondoka wote wakati Diamond alipokwenda Nigeria kwenye shoo ya Mwanasoka Bora wa Afrika 2014.

“Awali, Diamond alitaka akamlaze hotelini lakini mtoto wa kike akakataa, akasema anataka kuangusha usingizi nyumbani kwa mkwewe, Diamond akasema ruksa mama,” kilisema chanzo hicho.
Kikizidi kumwaga data, chanzo kilisema, mbali na kulala, Zari alishiriki kazi za ndani ikiwemo kupika na kupakua kama ilivyokuwa kwa zilipendwa wa Diamond, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Wema Sepetu.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo hakutaka kufafanua mengi zaidi ya kukiri kwamba mrembo huyo alikuja Dar na kuondoka naye.
Zarinah Hassan ‘Zari’ akiwa na 'Diamond Platnumz'.

“Wewe jua alikuja, nikaondoka naye hayo mambo mengine siwezi kuyazungumzia,” alisema Diamond.
Amani lilipomtafuta mama Diamond kwa njia ya simu hakupatikana lakini mtu wa karibu alisema kwa sasa hatumii simu kwa sababu ambazo hazikutajwa.

No comments: