Sunday, February 22, 2015

ASKARI WA JKT WAENDA KUMJULIA HALI MWENYEKITI WAO ALIYETEKWA

Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Askari wakiimarisha usalama eneo la Hospitali ya Muhimbili.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
Baadhi ya wanajeshi wa JKT wakiingia hospitalini.

VIJANA mbalimbali ambao walipata mafunzo kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), leo wamekutana katika eneo la Msimbazi Center jijini Dar es Salaam, kisha kuelekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kumjulia hali mwenyekiti wao George Mgoba ambaye alitekwa na watu wasiojulikana.

GPL ilifanikiwa kufika eneo la Msimbazi Center walipokusanyika askari hao na baadaye kuelekea Hospitali ya Muhimbili. Hata hivyo, wanahabari walishindwa kuzungumza na mwenyekiti huyo kwa sababu za kiusalama.

(Habari/Picha: waandishi wetu/GPL)

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake