Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Nd. Hemed Salum wa pili kutoka kulia akimpatia maelezo Balozi Seif aliyefika kukagua eneo la mawe mazito ambalo liko chini ya dhamana ya Mfuko wa Kuwahudumia Watoto Yatima Zanzibar Hapo Vitongoji Chake chake Pemba.Wa kwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Mwanjuuma Majid na Mwakilishi wa Kampuni ya Mecco Bwana Abdullkadir Mohamed Bujeti.
Mwakilishi wa Kampuni ya ujenzi wa Miundombinu ya Bara bara ya Mecco Bwana Abdullkadir Moh’d Bujeti akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif hatua iliyofikiwa ya kukamilika kwa ujenzi wa Bara bara Tatu zaMkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na OMPR, ZNZ.
Eneo la Mawe Mazito la Hecta 20 liliopo Vitongoji chake chake Pemba ndilo pekee lilobakia Kisiwani humo kwa ajili ya upatikanaji wa rasimlali ya jiwe kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa agizo kwa Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Zanzibar kuufutia hati ya matumizi ya ardhi Mfuko wa kuhudumia Watoto yatima Zanzibar { Zanzibar Children Fund } iliyopewa katika eneo la mawe mazito liliopo Vitongoji Chake chake Pemba.
Alisema eneo hilo la Hekta 20 ndilo pekee lililobakia Kisiwani Pemba linalotumiwa na Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano kwa ung’oaji wa mawe mazito yanayotumiwa katika miundo mbinu ya ujenzi wa mawasiliano ya Bara bara.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofanya ziara fupi ya kukagua eneo la Mawe mazito na kuiagiza Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati kufanya utaratibu mara moja wa kuupatia sehemu nyengine Mfuko huo ili uendelee na malengo yake iliyojipangia.
Alisema uamuzi huo wa Serikali umekuja baada ya eneo la Hekta 133 lililotengwa na Serikali kwa ajili ya shughuli ya uchimbaji mawe mazito Kisiwani Pemba kumalizika kwa rasilmali hiyo muhimu kwa ujenzi wa miundo mbinu ya bara bara.Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisisitiza kwamba Ardhi ni Rasilmali ya Taifa.
Hivyo Serikali wakati wote ina haki na wajibu wa kulitumia eneo la Ardhi popote pale Nchini kwa maslami ya Jamii nzima.Mapema Afisa Mdhamini Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Pemba Nd. Hemed Salum alisema kwamba eneo hilo la Hecta 20 za ardhi walizopewa Mfuko huo wa Kuhudumia Watoto Yatima Zanzibar ni miongoni mwa Hekta 133 zilizotengwa maalum ya Serikali kwa kazi ya uchimbaji wa Mawe mazito.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata wasaa wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa Bara bara ya Wete Gando na Gando Ukunjwi unaosimamiwa na Kampuni ya Mecco ambapo Mwakilishi wa Kampuni ya MECCO Bwana Abdullkadir Moh'Bujeti alimueleza Balozi Seif kwamba wahandisi wa ujenzi wa Bara bara hiyo wanaendelea na harakati za ujenzi katika kiwango cha kuridhisha.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake