Monday, February 23, 2015

MKUU WA MKOA WA TANGA AUSIFU MFUKO WA GEPF KWA UBUNIFU NA HUDUMA BORA KWA WATEJA

Meneja Masoko wa Mfuko wa GEPF,Aloyce Ntukamazina (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi na kumkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Magalula Saidi Magalula (katikati) kufungua semina maalum kwa maafisa rasilimali watu wa Mkoa wa Tanga,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Tanga Beach Resort,jijini humo.wa kwanza kushoto ni meneja wa GEPF mkoa wa Tanga,Silvanus Aloyce.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Magalula Saidi Magalula akifungua rasmi semina hiyo maalum kwa maafisa rasilimali watu wa mkoa wa Tanga pamoja na wilaya zake.
Baadhi ya maafisa rasilimali watu wakifuatilia kwa makini mada zilizotolewa na Mfuko wa GEPF.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Magalula Saidi Magalula akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka GEPF pamoja na maafisa rasilimali watu waliohudhuria semina hiyo maalum.
Mmoja kati wa maafisa rasilimali watu akifurahia jambo na afisa wa GEPF mkoa wa Tanga,Baraka Mtoi wakati akijiunga na mpango wa hiari wa kujiwekea akiba (VSRS).

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake