ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 20, 2015

Dk Shein akutana na watendaji wa wizara ya Fedha

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Fedha katika mkutano wa siku moja uliozungumziautekelezaji mpango kazi wa Wizara ya hiyo kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,


Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha wakimsikiliza Waziri wa Wizara hiyo Omar Yussuf Mzee(hayupo pichani) alipokuwa akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 katika mkutano uliofanyika leo asubuhi ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar mbele ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Khamis Mussa (kushoto) na watendaji wengine wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Utekelezaji wa mpango kazi wa Wizara kwa kipindi cha mwezi Julai-Disemba 2014 iliyotolewa na Waziri Omar Yussuf Mzee (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo asubuhi chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.]

No comments: