ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 20, 2015

UKIZIJUA MBINU HIZI, MAUMIVU YA MAPENZI UTAYASIKIA TU

Mapenzi ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine. Unahitaji kuielewa vizuri sanaa hiyo ili uweze kuishi vyema na mwenzi wako. Kama ilivyo kwenye upigaji wa gitaa, ili ulipige vizuri na kuweza kutoa muziki mtamu, ni lazima ujifunze.

Vivyo hivyo kwenye mapenzi, ili uishi kwa amani na furaha na mwenzi wako, ni lazima ujifunze mambo muhimu ya kuzingatia ambayo ukiyafanyia kazi, kamwe hutakuja kukutana na maumivu ya mapenzi.

1. KUWA MKWELI
Miongoni mwa mambo yanayoweza kukufanya ukaishi vizuri na mwenzi wako, ni kuwa mkweli katika kila unachokifanya kuanzia kwenye maisha yenu ya kimapenzi mpaka kwenye maisha ya kawaida.
Wengi huwa hawaoni umuhiku wa kuwa wakweli kwa wenzi wao kwa kuamini kuwa hilo ni jambo dogo ambalo haliwezi kuathiri uhusiano wa watu wawili kwa namna yoyote. Kuamini hivyo ni makosa, mapenzi ya kweli yanajengwa katika ukweli, jitahidi kuwa mkweli kadiri uwezavyo utaona raha ya mapenzi.

Ipo imani kwamba eti wanawake wengi wanapenda kudanganywa ili wadumu kwenye mapenzi, binafsi sikubaliani na hili, ukweli utamfanya mtu aridhie mwenyewe namna ya kuishi na wewe kuliko kuendelea kumlaghai kwa maneno mengi ya uongo kila siku.

2. KUWA MWAMINIFU
Pengine hii ndiyo siri kubwa kuliko zote kwenye uhusiano wa kimapenzi. Tunaishi katika ulimwengu unaokwenda kasi sana, teknolojia na mambo ya kisasa yanatubadilisha mfumo wa maisha yetu na kujikuta tukiwa kwenye hatari kubwa ya kuchepuka na kuwaumiza wenzi wetu.

Mtu yeyote anayejitambua na kuelewa anataka nini kutoka kwa mwenzi wake, kamwe hawezi kumsaliti kwa kutoka na mtu mwingine kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kukata tawi la mti ulilokalia.
Hata kama leo hajajua, umechepuka na kufanya kuwa siri yako, ipo siku atajua na pengine huo ndiyo utakuwa mwisho wa uhusiano wenu au mwanzo wa safari chungu ya kimapenzi. Kuwa makini, baki njia kuu.

3. MHUDUMIE
Hii inawahusu zaidi wanaume, kama upo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke ambaye kweli unampenda na unataka kudumu naye maisha yako yote, jitahidi kadiri uwezavyo kumtimizia mahitaji yake muhimu.

Hulka ya mwanamke ni kwamba hata kama yeye anafanya kazi na ana mshahara mkubwa kuliko wewe, bado atataka umsaidie kwenye mambo mbalimbali yanayomhusu. Ukimtatulia shida zake, hata kama ni ndogondogo, atajiona yuko sehemu salama na kuzidisha mapenzi kwako, hataona sababu ya kuwa na mwingine wakati unamtimizia kila kitu.

4. MRIDHISHE
Siri nyingine kubwa katika uhusiano wa kimapenzi wa watu wawili, ni kila mmoja kujua namna ya kumridhisha mwenzi wake na kukidhi haja kikamilifu muwapo faragha.

Tendo la ndoa linalofanywa kikamilifu, linatajwa kuwa na nguvu ya kuwafanya wahusika kuzidi kupendana na kuwa karibu zaidi, hata kama watakuwa wanapitia katika misukosuko ya maisha. Jifunze namna ya kumridhisha mwenzi wako kikamilifu muwapo faragha.

GPL

No comments: