Katibu wa Halmashauri Kuu (Nec), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) Taifa, itafanya kikao cha kawaida cha siku moja Jumamosi ijayo, huku hatima ya makada sita wa chama hicho, akiwamo Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, kama walitimiza au la masharti ya adhabu ya kifungo cha miezi 12 waliyopewa na Chama, ikitarajiwa kujulikana baada ya kikao hicho cha CC.
Pia inatarajia kutoa hatima ya Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Prof. Anna Tibaijuka, Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja na Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge.
Prof. Tibaijuka, Ngeleja na Chenge, wote kwa nyakati tofauti walihojiwa na Kamati ya Maadili ya CCM, iliyopo chini ya Mwenyekiti wake, ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Bara, Philip Mangula, kwa tuhuma za kupokea fedha zinazodaiwa kuwa ni sehemu ya zaidi Sh. bilioni 300 zilizochotwa kifisadi katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania.
Adhabu hiyo ilitolewa dhidi ya makada hao kwa kutuhumiwa kufanya vitendo vinavyoashiria kuanza kampeni za kutaka wateuliwe na chama hicho kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, kabla ya wakati.
Makada wengine waliotumikia adhabu hiyo iliyomalizika Februari 18, mwaka huu ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe; Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye; Mbunge wa Sengerema, Ngeleja; Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.
Adhabu hiyo pamoja na mambo mengine, ililenga kuwachunguza makada hao pamoja na kutakiwa kujirekebisha.
Pia kamati ndogo ya udhibiti iliagizwa kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja kanuni za Chama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Halmashauri Kuu (Nec), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kikao hicho cha CC-CCM ni cha kawaida na kwamba kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa vikao vya utangulizi kwa ajili ya maandalizi ya kikao hicho vinaendelea kukamilishwa.
Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza wazi ajenda zitakazojadiliwa katika kikao hicho.
Alipoulizwa na NIPASHE jana kujua ajenda za kikao hicho, Nape alisema:
“Taarifa mliyotumiwa kuhusu hicho kikao ndivyo hivyo ilivyo, haina nukta wala koma.”
Hata hivyo, mwanzoni mwa wiki iliyopita, Nape alizungumza na NIPASHE na kusema CC-CCM ndiyo itatoa maamuzi kuhusu hatma ya makada hao baada ya kupatiwa taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa adhabu zao kutoka kwa Kamati ya Maadili ya Chama.
“Mara kadhaa mmeniuliza swali hili, CCM tunasema hivi, muda ukiisha taarifa mtapewa... kujua kama adhabu yao imeisha au la. Na kamati itakaa lini, hiyo siyo kazi yenu. Na mimi mwenyewe sijui kwa sababu kazi ya kutathmini adhabu za watu hao haiko katika ofisi yangu. Inafanywa na taasisi nyingine ndani ya Chama,” alisema Nape.
Aliongeza: “Na kifungo chao kitajulikana baada ya tathmini ya Baraza hilo la Maadili ambalo ikumbukwe kwamba kazi hiyo ya kutathmini haishi ndani ya siku moja. Inaweza kuwa siku mbili, wiki moja, au miezi kwa sababu kanuni haitubani. Na baada ya kumalizika itapelekwa kwenye Kamati Kuu ambayo ndiyo itatoa maamuzi.”
Nape aliongeza kuwa tathmini ndiyo itaamua juu ya adhabu hizo kulingana na utekelezaji wao katika adhabu walizokuwa wamepewa kama wametekeleza ipasavyo au la.
Lowassa, Makamba, Ngeleja, Wasira, Sumaye na Membe, walipewa adhabu hiyo na CC-CCM Februari 18, mwaka jana, kwa madai ya kukiuka kanuni za uongozi na maadili za CCM, toleo la Februari, 2010, Ibara 6 (7) (i).
Februari 13, mwaka huu CC-CCM chini ya Rais Kikwete, ilifanya kikao chake Kisiwandui, Zanzibar na kuagiza adhabu kali zichukuliwe dhidi ya wale watakaobainika kuwa walikiuka masharti ya adhabu waliyopewa.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment